MPOLI PICTURES

I am a Writer

MPOLI PICTURES

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films. Our shooting style is journalistic, inconspicuous and centered on documenting each important moment as it happens. We dedicate our work to creativity, superior quality, exceptional quality and honest value in photography. Choose us to create your memory.

  • Morogoro, TANZANIA
  • +255714845658,
  • mpolipictures@gmail.com
  • www.mpolipictures.net
Me

My Professional Skills

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films.

Camera Opparating 90%
Camera Setting 70%
Video Shooting 95%
Graphics 90%
Showing posts with label Music. Show all posts
Showing posts with label Music. Show all posts
  • Mwana FA kwenye Nyimbo yake mpya…- ‘Asanteni kwa Kuja’ (Audio) Isikilize hapa

    Kama umepita mitandaoni ndani ya kama wiki mbili hivi au zaidi utakubaliana na mimi kwamba kulikuwa na trend ya picha ya Mwana FA ikituweka tayari kwamba jamaa anakuja kivingine.

    Jina lake ni Hamis Corleone Mwinjuma, kwenye stage ya muziki anafahamika kama Mwana FA… kaja na mdundo mwingine ambao umeachiwa leoleo… nakukaribisha kwenye link hii mtu wangu, unaweza kuisikiliza kwenye link ya Mkito

    BOFYA HAPA KUSIKILIZA- Mwana FA- ‘Asanteni kwa Kuja’
  • Drake na Craig David wanafanya mixtape pamoja.

    Msanii kutoka Uingereza Craig David ameweka wazi kuwa anarudi kwenye muziki hivi karibuni na kwamba atafanya mixtape yake na Drake.
    Craig anasema hajaanza kurekodi muziki bado ila maongezi na rapa huyu yanaendelea vizuri.
  • Adele anakabiliwa na kesi ya kuiba wimbo wa msanii aliyefariki miaka 15 iliyopita,mke wake yuko hai.

    Mwimbaji kutoka Marekani Adele anakabiliwa na kesi ya kuiba wimbo wa msanii kutoka Turkey anayefahamika kama Ahmet Kaya. Msanii huyu anasema wimbo wa Adele ‘Million Years Ago, kutoka kwenye album yake mpya ya ’25’ umefanana kabisa na wimbo wa miaka ya 80 wa msanii Ahmet Kaya unaoitwa Acilara Tutunmak (or Clinging to Pain).
    Wimbo huu ulifanyika mwaka 1985 na msanii huyu alifariki miaka 15 iliyopita.
    Kwa mujibu wa BBC, mke wa msanii huyu Gulten Kaya amesema haya kuhusu tuhuma hizo “It is unlikely that she would do such a thing. However, if she consciously did it, then it would be theft,”.

  • D’Banj akubali mchango wa Jose Chameleone kwenye muziki,na wasanii hawa pia.

    sanii kutoka Nigeria D’Banj ameongelea mchango wa Jose Chameleone kwenye muziki Africa na kusema ni mtu mwenye ushawishi mkubwa.

    D’Banj alikuwa Kampala hivi karibuni anasema anamuhishimu sana Jose Chameleone na anajua mchango wake katika muziki Africa. D’Banj anasema anamjua mshindi wa tuzo ya BET Eddy Kenzo ila hakujua anatoka Ugandan.

    D’Banj alimtaja Bebe Cool kama baba wa muziki na kusema anamjua kabla yeye hajawa maarufu,wasani wengine waliotajwa ni pamoja na Radio na Weasel na kusema alifahamiana nao mwaka 2011.

  • Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani

    Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani. Duru zinaarifu kuwa mshindi huyo wa tuzo ya Oscar pamoja na rubani wake walinusurika kufariki baada ya ndege waliokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu lake ilipokuwa ikikwenda kwa kasi kabla ya kupaa angani.

    Ndege hiyo ya kibinafsi ililazimika kutua mjini Tunica takriban kilomita 65 kutoka Clarksdale, Mississippi ilikopoteza mwelekeo na kwenda nje ya barabra maalum ya kutua.

    Katika taarifa aliyotuma kwa vyombo vya habari, Nyota huyo nguli wa ''The Shawshank Redemption ''alisema ''wakati mwengine mambo huenda mrama kwa hivyo kilichotokea leo ilikuwa mlipuko wa gurudumu ambayo ilisababisha hitilafu zaidi''

    Hata hivyo namshukuru rubani wangu Jimmy Hobson tulitua salama wa salmin. "Ndege bila shaka iliharibika hata hivyo nashukuru kwa wale walioniombea mimi ni mzima wa afya'' alisema bwana Freeman .

    Msanii huyo mwenye umri wa miaka 78 amewahi kuteuliwa kwa vitengo 7 vya tuzo za Oscar katika filamu alizoigiza Driving Miss Daisy, Street Smart na Invictus. Alituzwa mwaka wa 2005 kwa mchango wake katika filamu ya 'Million Dollar Baby'.
  • Baada ya kuitwa ‘Underground’ Fid Q asema haya.

    Fid Q ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kueleza kwamba tukio hilo lilitokea siku ya tamasha la Wizkid Live In Dar, alipoenda kufanya sound check kabla ya onesho kuanza.

    “Mimi na bendi yangu tulifika pale mapema kwa ajili ya masuala ya Sound Check, kwanza ilitangulia bendi yangu wakawa wanazungushwa sana kufanya sound check, ikabidi niende mwenyewe, jamaa akaniambia mtafanya sound check, mi ikabidi nimfuate jamaa nikamwambia vipi mbona sisi tumefika mapema lakini hatufanyi sound check, akaniambia take it easy man, those guys with big names they deserve to do sound chek alafu nyinyi ma underground mtafuatia“, alisema Fid Q akielezea jinsi tukio lilivyokuwa.

    Fid Q aliendelea kusema kwamba baada ya kitendo hicho alienda kuieleza bendi yake na kuanza kucheka, lakini ni kitendo kilichompa changamoto.

    “Basi mi na bendi yangu tukabaki tunacheka tukaipenda, bendi yangu ikaniuliza unajisikiaje kuhusiana na hicho kitu!? nikasema jamaa kanifurahisha kwa sababu ye anajua watu ambao anawaona katika TV za kimataifa, wengine sisi hatuonekani kwa hiyo kanikumbusha mi bado nina localy, kwa hiyo nina kazi kubwa ya kujipromote kimataifa, kwa hiyo nimechukulia kauli yake kama challenge na jamaa hajakosea“, alisema Fid Q.
  • Christian Bella amesema wimbo aliofanya na Alikiba utachelewa kuachiwa kwakuwa walikubaliana kuanza na video

    Christian Bella amesema wimbo aliofanya na Alikiba ‘Nagharamia’ utachelewa kuachiwa kwakuwa walikubaliana kuanza na video. Bella amesema wameamua kuonjesha tu wimbo huo ili kuwatoa hofu mashabiki wanaoisubiria kazi hiyo kuwathibitisha kuwa ni kweli wameshaurekodi.

    “Tulikubaliana kushoot video ndio tutoe kazi,” amesema Belle.

    “Kwahiyo hatujapata nafasi ya kushoot video. Labda tutaondoka Jumatatu kwenda kushoot video tumejipanga sijui kama kutakuwa na mabadiliko yoyote. Watu wameisubiria sana, kwangu mimi nilikuwa nashindwa hata kuongelea. Unajua ukifanya kolabo unakuta mwenzako yupo busy, akipata nafasi na wewe unakuwa busy,” alikiambia kipindi XXL kupitia Clouds FM.

    “Kwahiyo kutoa teaser hiyo ni kuwafanya watu waelewe kazi ipo na wasione kama ilikuwa longo longo. Ila sijapromise watu kwamba inatoka lini, kwa sababu tunapishana sana kuhusu ratiba, tunashindwa kupata nafasi. Kwahiyo kusema kweli sijui tutaitoa lini. Kwahiyo ninachoomba mimi ni tupate nafasi tukafanye video ikifanyika ndio tutajua.”
  • Rapa Rick Ross kataja jina la album yake mpya,itakuwa ya mwisho chini ya Def jam.

    Baada ya kutoa mixtape yake ya ‘Black Dollar’ rapa Rick Ross  ametangaza jina la album yake mpya ambayo amesema itaitwa Black Market.

    Rick Ross amesema kwenye interview kuwa album hii ni muendelezo wa mixtape yake.Akiongelea kazi hii Rozay amesema hii ni Project ambayo ni ya Next Level, Hii pia itakuwa album ya mwisho kupitia lebel ya Def Jam na itatoka December 2015.

    Rafiki Na Shabiki Wangu, Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori Zote Kutoka Kwangu Instagram , Twitter Na Facebook

    FahamuTv ni sehemu nyingine ya kutazama na kusikiliza Interview za mastaa, Bonyeza hapa KuSubscribe



  • Umoja uliopo kati ya Weusi, Navy Kenzo, Vanessa na Jux haukupangwa – Nahreel

    Wasanii wa kundi la Weusi, Navy Kenzo pamoja na Vanessa Mdee na Jux wana familia yao ‘Good Music family’ ambayo hushirikiana katika kazi zao mbalimbali za sanaa.

    good music family

    Producer wa The Indusrty ambaye pia ni msanii wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel amesema kuwa umoja wao huo haukupangwa na wahusika bali ni kitu kilichokuja chenyewe kupitia studio yake ya The Industry.

    “Sisi sio kwamba tulipanga tulikaa chini no, nadhani the Industry imeweza kuleta watu wote karibu ikatengeneza ikawa kama familia. Na sisi wote ni watu wenye nia nzuri tunapenda mziki, ndio maana tumekutana tukasema tunaenda pamoja.” Alisema Nahreel kupitia Planet Bongo ya EA Radio.
  • Rich Mavoko - Msanii kuonesha mali zake mtandaoni ni kutoa shukurani kwa mashabiki

    Watu maarufu wamekuwa na kawaida ya kushare mambo yao katika mitandao ya kijamii, hii ikiwa ni pamoja na maisha binafsi na kuonesha mali walizochuma kupitia kazi zao.

    Watu maarufu wamekuwa na kawaida ya kushare mambo yao katika mitandao ya kijamii, hii ikiwa ni pamoja na maisha binafsi na kuonesha mali walizochuma kupitia kazi zao.

    mavoko

    Kwa mastaa wa bongo, baadhi yao hawapendi ‘kuringishia’ mali zao mitandaoni huku wengine akiwemo staa wa muziki Rich Mavoko wanaunga mkono tabia hiyo.

    Mavoko anaamini kwa kuonesha mali anazomiliki mtandaoni ni kutoa shukurani kwa mashabiki.

    “Mtu mwengine inawezekana anapost vitu au nyumba, au gari au pesa, kwa kutoa shukrani kwa watu ambao wamemfanya mpaka awe hapo, ina maana ni hao watu ndio anaowapostia, ili waone kwamba sasa hivi nimepiga hatua kiasi gani.” Alisema Rich Mavoko kupitia Planet Bongo ya EA Radio.
  • Lil Wayne amshtaki Birdman akimtaka amlipe dola milioni 51. adai Birdman amewaibia Drake, Nicki Minaj na Tyga mkwanja mrefu

    Ugomvi kati ya Young Money na Cash Money unaendelea kuwa mkubwa zaidi baada ya Lil Wayne kutoa madai mapya.

    birdman-wayne-nicki-drake

    Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Wayne anadai kuwa na maelezo kutoka kwa wawakilishi wa Drake na Tyga yakisema wameibiwa fedha nyingi.

    Kwa upande wa Nicki Minaj, anadai kuwa Young Money imemfanyia uhuni kwa kushindwa kuwalipa maproducer. Young Money inadai kuwa jukumu la kuwalipa watayarishaji lilikuwa la Cash Money.

    Young Money imesema inadai fedha kibao kutoka kwenye dola milioni 100 ambazo Cash Money ilipewa na Universal.

    Hata hivyo timu ya Birdman imejibu kuwa tayari fedha hizo zimelipwa ambapo dola milioni 20 zilienda kwa Young Money mwaka 2012, milioni 12 zingine zikienda kwenye album ya Lil Wayne na zingine milioni 70 zikilipwa kama advances.

    Cash Money wanadai kuwa wasanii wa Wayne walitakiwa watengeneza album 21 lakini wametengeneza 13 tu.

    January, Wayne alimshtaki Birdman akimtaka amlipe dola milioni 51.
  • UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE NI LE0 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, WAIMBAJI WATAKAO MSINDIKIZA WATAMBULISHWA


    Boniface Mwaitege, atakaye zindua albamu zake tatu hapo kesho
    Faustine Munishi, mmoja wa waimbaji wa injili atakayetoa burudani.
    Upendo Kilahiro, atatumbuiza.
    Jesca Maguba (BN), atatumbiza(VICTOR)
    Atosha Kissava, atatumbuiza.
    Mwimbaji wa nyimbo za injili, Boniface Mwaitege (katikati), akiimbaji sanjari na waimbaji wenzake wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi. Waimbaji hao kesho watatoa burudani wakati wakimsindikiza mwimbaji mwenzao Boniface Mwaitege katika uzinduzi wa albamu zake tatu za Utanitambuaje, Mama ni mama na Tunapendwa na Mungu utakaofanyika kesho ukumbi wa Diamond Jubilee saa nane mchana kesho. Kutoka kulia ni Faustine Mnishi, Upendo Kilahiro, Jesca Magupa (BN) na Atosha Kissava.
    Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi huo.
    Msama (katikati), akiwa na waimbaji watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo.
    ????????????????????????????????????
    Mwimbaji wa nyimbo za injili, Boniface Mwaitege (katikati), akiimbaji sanjari na waimbaji wenzake wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
    MWANAMUZIKI wa Injili, Boniface Mwaitege kesho mchana anatarajiwa kuzindua albamu zake tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mkurugenzi wa Kapuni ya Msama Promotion alisema kuwa maandalizi yote muhimu ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia saa nane mchana yamekamilika, Mwaitege atatambulisha albamu hizo kwa kusindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili.
    Alisema mashabiki wa muziki wa Injili watarajie burudani ya nguvu kutokana na maandalizi ya nguvu na ya kipekee aliyofanya mwanamuziki huyo ikiwemo kurekodi albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Nairobi na Kenya.
    “Maandalizi yote ya uzinduzi wa albamu za Mwaitege yamekamilika, mashabiki watarajie burudani ya nguvu, pamoja na ujumbe kutoka katika nyimbo hizo pamoja na mwanamuziki wengine watakamsindikiza,” alisema Msama.
    Alisema sehemu ya mapato katika uzinduzi huo ambao pia utafanyika katika mikoa mingine, itapelekwa kwa kwenye vitu vya watoto yatima.
    Msama alizitaja albamu hizo ni pamoja na ‘Tunapendwa na Mungu’ yenye nyimbo za ‘Tukiimba Mungu anashuka’, ‘Mtoto wa mwenzio ni wako’, ‘Safari Bado’, ‘Tumekuja Kukuchukua (Bibi harusi)’, ‘Tuko Salama’, ‘Moyo wa Shukrani’, ‘Hakuna Ridhiki’, albamu nyingine ni Utanitambuaje na Mama ni Mama.
    Baadhi ya wanamuziki watakaopanda jukwaani kusindikiza uzinduzi wa albamu za Mwaitege waliotambulishwa kwa waandishi wa habari na baadhi ya nyimbo zao zilizotamba katika mabano ni Upendo Kilahiro (Baba Ninakuabudu), Jesca
    Magupa (Napokea), Mchungaji Faustine Munishi (Malebo) na Atosha Kisava (Umwema).
    Akizungumzia utambulisho wa albamu zake tatu, Mwaitege alisema amejiandaa vizuri kwa uzinduzi huo, ambapo mashabiki wataweza kupata burudani nzuri na ujumbe, pia albamu hizo zitakuwepo ukumbini.
    Aliwataka mashabiki kufika kwa wingi katika onesho hilo ili kumpa hamasa yeye na waimbaji wengine ambao watamsindikiza.
    Awali wasanii wengine waliotajwa kusindikiza uzinduzi huo ni pamoja na John Lisu, Martha Mwaipaja, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Eiphraim Sekereti, Atosha Kisava, Mess Chengula, Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe na Joshua Mlelwa.
    Onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini.
    Kiingilio katika onesho hilo kitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti maalumu, sh. 5,000 na sh.2,000 kwa watoto.
  • Hii Kuhusu Collabo Ya Rapper Kutoka Ghana Na Fid q.


    Ni mara chache sana unasikia Fid Q anafanya collabo na msanii yeyote kutoka nje ya Tanzania. 

    Kwenye inteview na Efm Nov 20 1014, Diamond Platnum amesema amefanikiwa kumunganisha rapper kutoka Ghana Sarkodie na Fid q kutoka Tanzania baada ya kusikia Fid q angependa kufanya nae kazi. Diamond anasema alimtumia message Sarkodie ikiwa na clip ya show ya Fid q na jamaa alishanga shangwe la Fid q kutoka kwa mashabiki.
     
    Mpaka sasa Sarkodie ameshatumiwa wimbo ambao atafanya na Fid q ili asikilize na kufanya sehemu yake.
  • Picha,Tattoo Ya Ngwea Na Geez Mabovu Kwenye Kifua Cha Dark Master


    Rapper wakundi la Chemba Squad Dark Master ametengeneza kumbukumbu nyingine kwenye maisha yake kwa kujichora tattoo yenye majina ya marehemu Ngwea na Geez Mabovu.

    Akiwa ni member wa kundi alilokuwa Ngwea na mtu wa karibu wa Geez Mabovu Dark Master anasema hii misiba miwili ni pigo kubwa kwenye maisha yake.


  • Picha,Chris Brown Achora Mashairi Ya Wimbo Wa Tupac “Lord Knows” Kwenye Gari Yake'Lamborghini'


    Mchora tattoo anayefahamika kama Michael “Huero” amemsaidia Chris Brown kuchora mashairi ya wimbo anaoupenda wa 2 Pac wa 'Lord Knows' kwenye gari yake aina ya Lamborghini. 
     
     
     
     


  • New music Diamond Platnumz feat Usher Raymond!

    Diamond Platnumz is unstoppable! Ni muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia tetesi kuwa amerekodi ngoma na msanii mkubwa wa Marekani japo hakuwahi kumtaja, lakini sasa tunaweza kuwa na ubashiri sahihi!
    Muimbaji huyo alikuwa akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo asubuhi ambapo aliulizwa ni msanii gani wa nje ya Afrika anayependa kufanya naye kazi.

    Diamond alidai kuwa tayari msanii anayemkubali zaidi nchini Marekani ameshafanya naye kazi japo hakupenda kumtaja tena.

    Aliombwa amtaje msanii mwingine tofauti na huyo na kusema wasanii watano anaowapenda zaidi nchini Marekani niNicki Minaj, Chris Brown na Usher Raymond na kwamba mmoja kati ya hao tayari ameshafanya naye ngoma!

    Kwamujibu wa mtandao wa Bongo 5 wao wame bashiri kuwa kwakuwa inafahamika Diamond Platnumz anamkubali Usher Raymond basi inawezekana atakuwa ndiye msanii waliye fanya naye kazi hiyo.
  • Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO' akishirikiana na Msanii wa Kenya, Atemi

    Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO'.
    'Moyo' ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .
    Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.

    Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni 'single' ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.
    Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi 'Usijali' akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.

  • Nikki Mbishi atoa sababu za kubadili uamuzi wa kuacha muziki, kutoa wimbo mpya March 4

    Rapper Nikki Mbishi ambaye aliuanza mwaka 2015 kwa kufanya uamuzi uliowashtua mashabiki wengi wa Hip Hop baada ya kutangaza kuacha muziki, ametangaza kuachia ngoma mpya wiki ijayo.
     Baada ya kuulizwa sababu zilizomfanya abadili uamuzi wake na kuendelea kufanya muziki hizi ndio sababu alizozitoa, “Nimegundua kwamba bado watu wananidai vitu vingi sana ngoja kwanza labda nimalizane nao,” Nikki alisema kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

    “Nimeona response yao ambao walikuwa positive, nimeona watu wangapi niliwa disappoint nimeona watu wangapi yaani wamepoteza ari yao ya kushabikia muziki, vitu kibao. Kwahiyo wakongwe wenyewe wazee wameongea vitu kibao vimetokea kwahiyo ngoja tuone kinachowezekana.”

    Ngoma mpya ya Nikki Mbishi itatoka Jumatano ijayo (March 4) ambayo pia itakuwa ni birthday yake.
  • Rapper AKA wa South Africa Aeyafananisha mapokezi ya Diamond Dar na ya wasanii wakubwa kama Chris Broun na Justin Bieber

    AKA ni rapper maarufu kutoka Afrika Kusini ambae alishinda tuzo moja kwenye tuzo za Channel O 2014 hapa Johannesburg Afrika Kusini ambako Diamond alishinda tuzo tatu kwa mkupuo.

    Baada ya kuziona picha na video za jinsi Watanzania walivyompigia shangwe Diamond Platnumz kwenye mapokezi yake kuanzia Airport Dar es salaam, A.K.A ilibidi aandike haya maneno.

    Kaandika >>> ‘Diamond alirudi Tanzania baada ya ushindi wa tuzo tatu za Channel O, jaribu kufikiria watu wa South Afrika wangeguswa na Wasanii wao kama hivi, kwenye nchi yangu mapokezi kama haya ni kitu ambacho kimehifadhiwa kwa ajili ya kina Justin Bieber na Chris Brown…. hongera Diamond’

    Diamond lands back in Tanzania after winning 3 Channel O Awards and this happens … Imagine South Africans felt like this about their own artists … In my country this is something reserved for the Bieber’s and Breezy’s … Where is our pride? Where is our passion? Anyways … BIG UP DIAMOND’
    – AKA
    Ni ahadi yangu kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook
  • Diamond kurecord tena audio, video na wasanii wakubwa Africa

    Mwanzoni mwa mwaka huu msanii Diamond Platnumz aliiwakilisha Tanzania katika kampeni iliyokuwa ikihamasisha kilimo (One Campaign) na kufanya wimbo pamoja na video na wasanii wakubwa Africa.

    Diamond amepata nafasi hiyo kwa mara ya pili ya kufanya kazi na One Campaign na safari hii anaungana tena na wasanii wengine kutoka Africa kwa ajili ya kutengeneza wimbo unaopiga vita ugonjwa wa Ebola

    "Kwa taarifa ambazo nimezipata tutatumia beat ya we are the world, tutaimba na kushoot video" amesema Diamond
    Licha yakuchaguliwa kuwepo katika kugombani tuzo za hannel O, zitakazofanyika weekend hii  Diamnd pia amepata shavu
    la kutoa tuzo mojawapo

    "Channel O pia ntatoa Tunzo pale sa subiri uone vingereza vyangu vya kushoto kulia pale wakati natoa tunzo 


  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.