MPOLI PICTURES

I am a Writer

MPOLI PICTURES

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films. Our shooting style is journalistic, inconspicuous and centered on documenting each important moment as it happens. We dedicate our work to creativity, superior quality, exceptional quality and honest value in photography. Choose us to create your memory.

  • Morogoro, TANZANIA
  • +255714845658,
  • mpolipictures@gmail.com
  • www.mpolipictures.net
Me

My Professional Skills

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films.

Camera Opparating 90%
Camera Setting 70%
Video Shooting 95%
Graphics 90%
Showing posts with label Slider. Show all posts
Showing posts with label Slider. Show all posts
  • KINGUNGE AACHANA NA CCM RASMI LEO! ASEMA WATANZANIA WANAHITAJI MABADILIKO KWA SASA!


    Mwanasiasa mkongwe ambaye ni pia alikua kada maarufu wa chama cha CCM Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho cha siasa na amesema sababu kubwa ni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kwa sasa. 
    Amesema hatojiunga na chama kingine cha siasa ila anaamini vijana, kinamama, na watanzania wanahitaji mabadiliko na yeye yuko upande wa mabadiliko.
  • UEFA:Matumizi ya vilabu kuangaziwa

    Shirikisho la soka barani Ulaya linajiandaa kuondoa sheria ya mwaka 2011 itakayozuia vilabu kufanya matumizi ya ziada.

    Katika mahojiano na redio ya Ufaransa RTL,rais wa UEFA Michel Platini amesema kuwa sheria hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri lakini itapigwa msasa mishoni mwa msimu huu.

    Hatua hiyo inafuatia ripoti katika gazeti la Le Parisien siku ya jumapili iliosema kuwa kuna mabadiliko muhimu yatakayofanyiwa sheria hiyo.
     
                                                                  Viongozi wa UEFA

    Manchester City pamoja na kilabu ya PSG zilipigwa faini mwaka uliopita kwa kukiuka sheria hiyo.

    Baadaye mwandani wa rais wa vilabu vya Ulaya ambaye pia ni katibu mpanga ratiba Gianni Infantino aliithibitishia BBC kwamba mazungumzo kuhusu FFP na vilabu vikuu vya Ulaya yanaendelea huku marekebisho hayo yakijadiliwa.

  • Jordon Ibe kusaini mkataba mpya Liverpool

    JORDON Ibe yuko mbioni kusaini mkataba wa muda mrefu baada ya Brendan Rodgers kuamua kuingiza vijana kwenye kikosi cha msimu ujao.
     
    Liverpool walimpa Ibe ofa ya mkataba mfupi mwezi februari baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mechi za ligi hususani dhidi ya Everton na Tottenham.
     
    Dili hilo sasa limeshafikiwa makubaliano na Ibe ambaye amekosekana tangu apate majeruhi ya goti dhidi ya Besiktas februari 26
  • Nkurunziza aanzan kuwawajibisha waliojaribu kumpindua, Aanza na mawaziri 3

    Nkurunziza
    Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita.

    Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara.

    Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.
  • West Brom waitungua Chelsea kipigo kikubwa, Fabregas alimwa kadi nyekundu

    WEST Bromwich Albion ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Hawthorns imewafumua magoli 3-0 mabingwa wapya wa ligi kuu England, Chelsea.
    Magoli ya West Brom katika mechi hiyo pekee ya ligi kuu England usiku huu yamefungwa na Saido Berahino dakika ya 9′ na Berahino akaongeza la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 47.
    Bao la tatu limefungwa na 60′ na Chrus Brunt.
    Hata hivyo Chelsea walicheza pungufu kwa muda mrefu kwani Cesc Fabregas ameoneshwa kadi nyekundu dakika ya 29′ kipindi cha kwanza.
    Takwimu za mechi zinaonesha Chelsea wamemiliki mpira kwa asilimia 59 dhidi ya 41 za wenyeji wao, lakini wamepiga mashuti matatu tu yaliyolenga lango, wakati West Brom wamepiga mashuti 6.
  • Guardiola backing Barca to win Berlin final

    Bayern’s head coach Pep Guardiola (L), gives a ball to Barcelona’s Luis Suarez during the soccer Champions League second leg semifinal match between Bayern Munich and FC Barcelona at Allianz Arena in Munich.
    MUNICH, May 13- Bayern Munich coach Pep Guardiola is now backing his ex-club Barcelona to win the Champions League after his Bavarian giants bowed out 5-3 on aggregate in the semi-finals.

    Guardiola’s Bayern exited at the last-four stage for the second year running, despite ending Barcelona’s 18-game unbeaten run with a 3-2 semi-final, second-leg win in Munich.

    Bayern were given an early glimmer of hope in their bid to overturn a three-goal deficit in Munich when the unmarked Medhi Benatia headed home on seven minutes at the Allianz Arena.

    But Barca effectively booked their place in the Berlin final on June 6 when Luis Suarez twice set up Neymar to score for the visitors before half an hour had been played.

    Bayern produced a rousing second-half performance with goals by Robert Lewandowski and Thomas Mueller, but Barcelona advance to face either bitter rivals Real Madrid or Juventus in the final.

    Having won 16 titles as a player, then a further 14 in four years as head coach at the Camp Nou, Guardiola is backing Barcelona to claim their first European crown since 2011 at Berlin’s Olympic Stadium on June 6.

    “I want to congratulate my players, I am really happy to be their manager on a day like today,” said Guardiola, as Bayern denied Barcelona a first win in Munich at the fifth attempt.

    “But I hope Barcelona can now win their fifth Champions League title in Berlin.

    “You can only beat Barcelona when you take the ball away from them, with it they are so strong.

    “We didn’t make the most of our chances in the first leg, but here we did.

    “It wasn’t enough at the end of the day, but there you go.

    “I hope the Spanish league has the rights to be screened in Germany soon, so that fans here can appreciate what a good player Lionel Messi is on a regular basis.

    “He was a pleasure to coach when I was at Barcelona and he has demonstrated yet again what he can do.”

    The win over Barcelona ended Bayern’s four-match losing streak since winning the German league title for the 25th time a fortnight ago.

    “We won four titles last season, this year we have just one, but it has been a tough season with lots of injuries and despite that, my players still attacked at every opportunity,” enthused Guardiola.

    Bayern’s come-back win demonstrated how much they wanted to reach an 11th European Cup final, but it was too little, too late, after their emphatic first-leg defeat.

    “We believed in the miracle, but we couldn’t make it happen,” said Bayern captain Philipp Lahm.

    “It’s impossible to stop those Barcelona players for the whole 90 minutes.

    “We didn’t lose it today, but in the first leg.”

    Goal-scorer Mueller was a constant threat to the Barcelona defence and made good on his pre-match promise that Bayern would fight until the final whistle.

    “We played a really great game in the first half but we’ve made two mistakes in defence and have been too wasteful with our chances,” said Mueller.
  • MASHABIKI WA MAN CITY HAWAKUWA NYUMA KWENYE SIKU HII MUHIMU KWA YAYA TOURE





    Jana kiungo wa Manchester City alitimiza umri wa miaka 31 wakati akiwa ndani ya kikosi chake hicho kilichokuwa kikicheza na QPR kwenye uwanja wa Emirates.

    Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliingia uwanjani huku wakiwa wamebeba mabango ya kumpongeza kwa kufikisha siku yake hiyo muhimu kwake.

    Furaha ya kiungo hiyo ilitimia baada ya timu yake kuweza kuiadhibu QPR kwa jumla ya mabao 6-0 na kuifanya ishuke daraja.



  • Taifa stars yajifua kwa Cosafa

    Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaingia kambini Jumatatu wiki hii kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini baadae mwezi huu.

    Mazoezi hayo pia yatakuwa ni sehemu ya maandalizi ya kucheza michuano ya kufuzu kucheza kombe la Mataifa ya Afrika ( AFCON) na michuano ya CHAN mwezi Juni mwaka huu.

    Kocha wea Stars, Mart Nooij tayari amechagua wachezaji 28 aliowaita, wapo vijana wanaochipukia na wenye uzoefu katika michuano ya kimataifa.

    Nooij amesema wachezaji watakaporipoti kambini watapimwa afya zao na madakatari wa timu na kisha atachagua 20 watakaokuwa “fit” kwa ajili ya kuelekea Afrika ya Kusini.

    Wachezaji watakaoingia kambini ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).

    Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).

    Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).

    Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.

    Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.
  • Ubelgiji yainyima Burundi msaada

    Ubelgiji imesitisha msaada wa aina yoyote kwa Burundi, hasa uliokuwa ukifadhili uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

    Hayo ni kutokana na mapigano makali ambayo yanashuhudiwa kwa sasa nchini humo, kati ya polisi na raia wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.

    Ghasia zimekuwa zikitokea nchini humo tangu rais alipotangaza hatua hiyo ya kuwania tena kiti hicho kinyume na katiba ya nchi hiyo.
    Rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu

    Mchunguzi mmoja wa jumuia ya bara Ulaya, alisema juma lililopita kuwa, masharti ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu yameafikiwa.

    Bwana Nkurunziza anazindua kampeini yake ya kuwania kiti hicho hii leo Jumatatu.

    Umoja wa mataifa umeelezea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoitoroka Burundi.
    Waandamanaji wakipinga hatua ya Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa tatu

    Kufikia sasa zaidi ya watu elfu mia moja na hamsini wamekimbia nchi hiyo huku zaidi ya watu 19 wakiuwawa katika ghasia.
  • MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI ENG, CARLOS MKUNDI ATOA POLE KWA WAHANGA WA MAFURIKO

    Mwimbaji wa nyimbo za injili Eng Carlos Mkundi ametoa pole kwa wahanga wa mafuriko nchini hususani kwa wakazi waishio Dar es salaam.

    Mwimbaji  huyo anayetamba kwa kibao chake cha NIMETOKA MBALI  Ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kufuatia mafuriko yaliyoleta athari kubwa Mangwe jijini Dar es salaam na kuua watu kumi na moja na wengine kukosa makazi

    Eng Carlos amewasihi watumishi wa Mungu kote nchini kuiombea Tanzania dhidi ya majanga mbalimbali yanayoendelea kama ajali na mafuriko na kuwatia moyo  walioathiriwa na mafuriko jijini Dar Es Salaam


    Amesema watanzania wote kwa kushirikiana na watumishi wa Mungu pia  hawana budi kumwomba Mungu alete Mvua ya kiasi itakayowezesha kuotesha mimea kwa ajili ya mazao

    Hata hivyo ameitaka serikali kutoa elimu ya kotosha kwa watu waishio mabondeni na kuwatafutia maeneo mazuri  ili kupunguza maafa ya mafuriko hapa nchini
    Mafuriko yanazidi kuwa tishio kwa maisha ya watanzania walio wengi hasa kwa mikoa ya Dar Es Salaam, Morogoro na shinyanga.


  • Peter Moores sacked as England head coach following Strauss apppointment

    Peter Moores: Shown the door by England
    Peter Moores has left his role as England head coach.
    The announcement by the ECB came shortly after Andrew Strauss was confirmed in the newly-created role of director of England cricket.

    England Assistant Coach Paul Farbrace will take charge of the England team for the upcoming Test series against New Zealand while Strauss and the ECB consider their options for a long-term replacement.

    Moores' exit comes following the squad’s return from the tour of the West Indies, where England were held to a drawn series by their unfancied hosts – losing the final Test in Bridgetown by five wickets.
    England vs New Zealand

    May 21, 2015, 10:00am

    Live on Sky Sports 2
    Get Sky Sports Get a Sky Sports pass

    An ECB statement said: "Peter is a man of great integrity and has offered a huge amount to England cricket.

    "He is admired by the players, his colleagues at the ECB and right across the game and deserves both our deep thanks and the widest recognition for his commitment and contribution.

    "The last year has been a period of transition and rebuilding in which Peter has nurtured new talent, developed new players and laid the foundations for the new coaching structure to build on.

    "This decision has been made as we focus on the future and our need to build the right approach and deliver success over the next five years within a new performance structure."

    Moores was originally appointed as head coach back in 2007 after a disastrous Ashes tour resulted in the resignation of Duncan Fletcher.

    The two-year spell included Test series defeats to India (twice), Sri Lanka and South Africa but it was his relationship with batsman Kevin Pietersen which was reportedly the primary reason for his removal in January 2009.

    Moores returned to county cricket and was offered the role of Lancashire coach where he guided them to their first County Championship title since 1934.

    However, Moores was reappointed as head coach in April 2014, replacing Andy Flower in the wake of England’s Ashes whitewash in Australia.

    An encouraging 3-1 Test series victory over India followed a 3-2 defeat to Sri Lanka but Moores’ critics rounded on him again in the wake of an abysmal 2015 World Cup, in which England failed to progress from the group stage.

    Watch England v New Zealand, 1st Test, 10am May 21, Sky Sports 2
  • Basi la Dar Express lateketea kwa moto

    Linahesabika kama tukio jingine la Basi kuwaka moto katika rekodi za mabasi yaliyowaka moto yakiwa safarini nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.
    Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu baada ya kuongea na Mtandao wa millardayo ni kwamba basi hili la kampuni ya Dar Express liliwaka moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa abiria.
    Amesema  ‘Ni kweli basi la Dar Express saa saba mchana kwenye kijiji ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima, hakuna yeyote aliejeruhiwa‘

  • Bolt kushindana na Gutlin wa Marekani

    Usain Bolt hana tatizo la kushindana dhidi ya Justin Gatlin kwa kuwa anahisi kwamba marufuku ya miaka minne aliyopewa ilikuwa ya haki.

    Bingwa huyo mara mbili wa michezo ya Olimpiki hivi majuzi alilalama kuhusu mwanariadha mwengine wa mbio fupi kutoka Marekani Tyson Gay ambaye alipigwa marufuku kwa mwaka mmoja baada ya kupatikana amekula dawa za kusisimua misuli.

    ''Marufuku aliyopewa Tyson ilikuwa haitoshi na kutuma ujumbe mbaya'', alisema Bolt. ''Justin Gutlin alipigwa marufuku na akaihudumia kwa hivyo sina shida naye'',.

    Mkimbiaji huyo wa mbio fupi kutoka Jamaica atapambana na wawili hao wikendi hii katika mbio za 4 mara 100 katika mashindano ya relay huko Bahamas.

    Chanzo; BBC
  • Malkia Elizabeth apata kitukuu chengine

    Mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza Prince William amejifungua mtoto wa kike.

    Habari iliyotumwa kupitia kwa mtandao wa Twitter kutoka kwa ikulu ya Kensington ilisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa salama kalba ya saa mbili unusu saa za uingeeza.

    Mtoto huyo aliye na uzito wa kilo tatu nukta saba alizaliwa muda mfupi baada ya kuwasili kweny hospitali moja mjini London.
  • Ukawa waanza kugawana nchi

    Viongozi wa Ukawa
    Dar/Mikoani. Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano ya hadhara na mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa ushindi.

    Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.

    Chadema kilianza ziara zake mikoani wiki zilizopita baada ya kuzindua mkakati wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka kambi mkoani Kigoma kwa kile ilichokiita kuimarisha majimbo ya kimkakati.

    Sanjari na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia katika moja ya ngome zake, mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya kiushindi, kinahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.

    Jitihada za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa ni majuma kadhaa tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

    Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.

    ACT - Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kilihitimisha ziara yake ya kimkakati katika mikoa tisa inayoonekana kuwa ngome ya CCM, wiki iliyopita wilayani Bariadi, Shinyanga na kuvuna wanachama zaidi 6,000 katika mikoa hiyo.

    NCCR-Mageuzi ipo Kigoma

    Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema jana kuwa Ukawa ina mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya kuhakikisha inajiimarisha kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.

    Alisema siku 10 zilizopita, timu ya NCCR ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti - Zanzibar, Haji Hamis Hamad ilianza ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya mkoa huo yanaendelea kuwa ngome yake.

    “Kigoma nzima ina majimbo yetu ya kimkakati na Ukawa wameshatukabidhi sasa kilichobaki ni kufanya ‘political management’ (usimamizi wa kisiasa) katika kiwango kinachotakiwa.

    “Katika kikosi hicho, pia wamo Katibu Mwenezi, David Kafulila, Katibu Mkuu Mstaafu, Samuel Ruhuza na Kamishna wa Kagera, Peterson Mshenyela na wengineo,” alisema Nyambabe.

    Chanzo; MWANANCHI
  • Mashindano ya Magari: Kenya kutimua vumbi Tanzania-zig zag

    Gari la mashindano
    Mashindano ya mbio za magari ya Tanzania, yanayojulikana kama "Zig Zag" yanategemewa kufanyika mkoani Tanga, Kaskazini mwa Tanzania May 3 huku washiriki zaidi ya 40, wakiwemo Wakenya watatu wakishiriki.

    Washiriki 20 wanategemewa kuwa wenyeji akiwemo bingwa mtetezi, Gurpal Sandhu kutoka Arusha, kwa mujibu wa waandaaji.

    Washiriki kutoka Kenya waliothibitisja kushiriki ni Yusuf Pasta, ambaye anaendesha gari aina ya Subaru Impreza N10, Janmohamed Abdilatif na Farhan Khan, wote wakiendesha Subaru GCB.Wanategemewa kuwa na wasaidizi wao (navigators).

    Mbio hizo zinategema kuanzia Tanga Beach Resort kuelekea Pongwe, Mkanyageni na Mjesani na kurudi zilipoanzia.
  • YANGA NDIO MABINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA

    Mashabiki wa Yanga wakifurahia ushindi
    Klabu ya Yanga nchini Tanzania imekata mzizi wa fitina baada ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa mwaka 2014/2015. Ushindi ulioupata wa magoli 4-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ndio ulihitimisha safari ya Yanga na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika.

    Kwa sasa Yanga, ambao wamewavua Azam ubingwa huo, ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya CAF, wakiwa na kazi ya kuitoa Etoile du Sahel mapema mwezi ujao katika hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho.

    “Nimefurahishwa na kushinda taji la ligi kuu Tanzania, wachezaji wamejituma na wamefanikiwa”, amesema kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm.

    Amisi Tambwe kutoka Burundi, ambaye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita akiwa mchezaji wa Simba, alifunga hat-trick (magoli matatu) dhidi ya Polisi Morogoro huku Simon Msuva akitupia moja.

    Sherehe za kutwaa ubingwa huo ziliendelea hadi nje ya mitaa kadhaa ya Dar es Salaam kutokana na furaha ya mashabiki. Hata hivyo, Yanga haikukabidhiwa kombe kutokana na kuendelea kwa ligi.
  • Wenger na Mourinho warushiana maneno

    Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango lake.

    Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.

    Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.
  • SIMBA YAZIDI KUPOTEA YAPIGWA 2-0 NA MBEYA CITY

    MATUMAINI ya Simba SC kurudi kwenye michuano ya Afrika mwakani, jana yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

    Matokeo hayo, yanaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 42 za mechi 22.  Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 46, baada ya kucheza mechi 21.(P.T)

    Mbeya City ilipata bao lake la kwanza dakika za majeruhi kipindi cha kwanza, mfungaji Paul Nonga aliyemalizia pasi ya Deus Kaseke iliyompita beki Mganda, Juuko Murusheed. Mbeya City wameifunga Simba SC mabao 2-0 Sokoine jana Katika mchezo huo, Simba SC ilipata pigo dakika ya 23, baada ya beki wake tegemeo, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda, Joseph Owino. Isihaka, beki anayeinukia vizuri aliumia baada ya kugongana na Peter Mapunda.

    Mbeya City ilipata bao lake pili dakika ya 69, mfungaji Peter Mwalyanzi, aliyemalizia krosi Nonga aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Simba jana.

    Kikosi cha Mbeya City kilikuwa:

    Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Christian Sembuli, Juma Nyoso, Kenny Ally, Peter Mapunda/Hassan Kibopile dk77, Raphael Daud, Paul Nonga, Cossmas Freddy/Peter Mwalyanzi dk59 na Deus Kaseke.

    Simba SC:

    Peter Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Juuko Murusheed, Hassan Isihaka/Joseph Owino dk23, Abdi Banda, Jonas Mkude, Elias Maguli/Issa Abdallah dk56, Ibrahim Hajibu, Said Ndemla na Ramadhani Singano ‘Messi’.

  • Balotelli ndiye aliyebaguliwa zaidi EPL wajue na wengine katika ligi hiyo

    Mario Balotelli ndiye mchezaji aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza ,huku mchezaji huyo akipokea zaidi ya ujumbe 8000 ,asilimia 50 zikiwa ni za kibaguzi.

    Takwimu hizo za kushtua zimeripotiwa na Kick it Out ,ambao walibaini kwamba raia huyo wa Itali alilengwa sana katika mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck akipokea ujumbe 1700 asilimia hamsini zikiwa za kibaguzi.

    Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika kilabu ya Liverpool Daniel Sturridge pia alionekana kulengwa katika mitandao ya kijamii baada ya kupokea ujumbe wa 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye mwelekeo wa kijinsia.

    Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya Chelsea ndio kilabu iliobaguliwa zaidi kwa ujumbe 20,000 huku liverpool ikiwa ya pili na ujumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa ujumbe 12,000 huku Manchester City na Manchester United zikipokea ujumbe 11,000.

  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.