![]() |
Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani. |
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani.
Akihutubia
kongamano la chama hicho, Mugabe amesema kuwa kuna majaribio ya
kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini wajumbe hawawezi
kupokea hongo.
![]() |
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe |
Kwa hilo amesema kuwa atapambana na rushwa ndani ya chamana kukabiliana na maafisa wa chama ambao kazi yao ni kutoa hongo.
Hasira ya Mugabe iliokana na
madai ya njama ya kumuua yaliyotolewa dhidi ya naibu wake Joyce Mujuru.
Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Chama tawala cha Zimbabwe
kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusu ni nani atakayerithi
nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ameilongoza taifa hilo tangu
lijinyakulie uhuru.
Vilveile kiongozi huyo ametupilia mbali dhana ya kujiuzulu akisema ni upuzi .
Hivi
karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliambia BBC
kwamba Mugabe amwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya mali yake binafsi.
Bwana Gumbo alisema kuwa lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.
Bi
Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye
anegchukua uskani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hio kutoka mikononi mwa watwala wazungu.
0 comments:
Post a Comment