MPOLI PICTURES

I am a Writer

MPOLI PICTURES

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films. Our shooting style is journalistic, inconspicuous and centered on documenting each important moment as it happens. We dedicate our work to creativity, superior quality, exceptional quality and honest value in photography. Choose us to create your memory.

  • Morogoro, TANZANIA
  • +255714845658,
  • mpolipictures@gmail.com
  • www.mpolipictures.net
Me

My Professional Skills

We are a full-service wedding cinematography and photography company. We create cinematic and documentary style wedding films.

Camera Opparating 90%
Camera Setting 70%
Video Shooting 95%
Graphics 90%
Showing posts with label Transfer News. Show all posts
Showing posts with label Transfer News. Show all posts
  • ANTHONY MARTIAL AMEZUNGUMZIA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU UHAMISHO WAKE

    Mchezaji mwenye miaka 19 ambae kwa sasa ni moja kati ya wachezaji wanaotegemewa sana na Manchester united kwa mara ya kwanza amezungumzia jinsi movement za uhamiso wake ulivyofanyika.

    Martial alisema,”Kwa ufupi mimi niliambiwa siwezi kuhama club ya Monaco kwa sasa, kwa hiyo akili yangu ikabaki kuwa nitaendelea kucheza Monaco”

    “Nilivyoambiwa kuna offer imekuja, sikusita hata sekunde na nakumbuka ulifanyika kwa haraka sana. Mimi nilitaka kuendelea kucheza kwenye Champions League”

    “Van Gaal alinipigia simu na akaongea na mama yangu ambae alinitafsiria walichozungumza. Nilivyofika Manchester nikakutana nae na kulikua na mazungumzo kwa kirefu zaidi na mambo yakafanyika haraka”

    Kuhusu media kuandika mambo mengi kuhusu uhamisho wake na familia yake kwamba ana umri mdogo lakini ana familia tayari, “Haikunisumbua kitu, labda kwa familia yangu na hayo yote ambayo yalikua yanaandikwa kwenye magazeti. Mimi nilitaka kufika haraka Manchester na kuanza kucheza soka”

    “Najaribu kupotezea hayo mambo ya media nakuendelea ku-focus kwenye soka na kujifunza English haraka iwezekanavyo”
  • KIMBEMBE : Kocha Louis Van Gaal apanga kuwachuja mastaa Man Utd


    MASTAA wa Manchester United watapata nafasi ya mwisho ya kuhakikisha wanamshawishi kocha Louis van Gaal ili kupata namba kwenye kikosi cha msimu ujao wakati itakapopigwa mechi ya wenyewe kwa wenyewe uwanjani Old Trafford.

    Man United imekamilisha ziara yake ya Marekani ambapo mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Paris St Germain jana Alhamisi asubuhi ulimalizika kwa kichapo cha mabao 2-0 na sasa timu hiyo itarudi Manchester kusubiri Ligi Kuu ianze.

    Awali, Van Gaal alikuwa amefuta mechi za kirafiki ndani ya Old Trafford, lakini sasa ameibuka na staili mpya ya kukigawa kikosi chake katika vikosi viwili ambavyo vitacheza mechi na hapo atachagua timu moja itakayomenyana na Tottenham Hotspur kwenye Ligi Kuu England Agosti 8.

    Kocha huyo atatumia mechi hiyo kupata wakali wa kuanza katika mechi hiyo ya kwanza ya Ligi Kuu na naamini itampa muda mzuri kutokana na ushindani wa namba uliopo kwa sasa. Van Gaal hataki kurudia ya msimu uliopita ambapo alivuna pointi 13 tu katika mechi 10 za mwanzo.

    Vikosi hivyo, kikosi cha kwanza kitakuwa na mastaa De Gea; Darmian, Jones, Blind, Shaw; Schneiderlin, Carrick; Mata, Depay, Young na Rooney na kikosi cha pili kitaundwa na Romero; Smalling, Blackett, McNair, Rojo; Schweinsteiger, Fellaini; Valencia, Herrera, Januzaj na Wilson.

  • USAJILI LIGI KUU BADO WIKI MOJA KUFUNGWA, SIMBA WASOTEA SAINI YA MAVUGO, YANGA…


    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    DIRISHA la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa tarehe 06 Agosti, 2015.

    Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho.

    Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 06, hakuna klabu au timu yoyote itakayoweza kufanya tena usajili wake, hivyo ni vyema vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya mwisho.

    Simba SC inasotea uhamisho wa Laudit Mavugo kutoka Vital'O

    Wakati ikiwa imebaki wiki moja usajili kufungwa, Simba SC inahangaika kumalizana na klabu ya Vital’O ya Burundi juu ya mshambuliaji Laudit Mavugo ambaye tayari imemsainisha Mkataba wa miaka miwili.

    Watani wao Yanga SC, nao wanataka kuboresha kikosi chao cha baada ya kutolewa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

  • IFAHAMU CLUB ALIYOSAINI DIDIER DROGBA


    Baada tetesi nyingi kuhusu wapi ataenda legend wa Chelsea hatimaye tetesi hizo zimeisha.Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amesaini mkataba wa miezi 18 ambao una thamani ya $3 million kwa mwaka.Club mpya ya Didier Drogba ni Montreal Impact ambayo inashiriki ligi ya Marekani.

  • BENZEMA ATOA MAJIBU KWA WALIODHANI ANAELEKEA ARSENAL


    Karim Benzema ali-post picha akiwa ndani ya private jet na kuandika “let the past remain the past, toward the future.
    Watu wengi waliichukulia hiyo post kwamba Benzema amepanda ndege kuelekea kujiunga na Arsenal. Ukizingatia wachezaji wenzake walikua wanapanda ndege kuelekea Shangai China.
    Story hii ilisambaa sana jana lakini leo Benzema ame post picha kwenye istagram na kuandika kwamba hivi sasa yupo Shanghai China na club yake ya Real Madrid. So, Benzema hakupanda ndege kuelekea uingereza kujiunga na Arsenal.
    2

    33
    444
  • ZLATAN YUKO TAYARI KUKIPIGA MAN UNITED, ILA ANAHOFIA JAMBO MOJA


    Mshambuliaji msumbufu na mwenye majivuno, Zlatan Ibrahimovic maarufu kama ‘Cadabra’ amesema angependa kuichezea Manchester United siku moja lakini anahofia ‘ngumi’ za kila siku na kocha Louis Van Gaal.

    Akiwajibu waandishi wa habari kama yuko tayari kujiunga na mashetani hao wekundu, Cadabra alisema angeweza kuchezea United lakini anahofia ugomvi wa kutoisha baina yake na Louis Van Gaal.

    Zlatan na Van Gaal hawakuwa na mahusiano mazuri tangu wakiwa Ajax miaka ya 1990’s lakini moto uliwaka zaidi baada ya Zlatan kumtaja Van Gaal kama ‘pampasi’ katika kitabu chake.

    Wawili hao hawana urafiki na kwamba hawawezi kuiva chungu kimoja. Hisia zimekuwa ni nyingi miongoni mwa mashabiki mara baada ya kocha Louis Van Gaal kutangaza kwamba atafanya usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji siku za usoni.

    Hata hivyo Cadabra nahodha wa Sweden anahusishwa na tetesi za kujiunga na AC Milan ya nchini Italia. Habari zinasema Zlatan amechoshwa na quality ya ligi nchini Ufaransa na sasa anafikiria kuihama klabu yake ya Paris St. Germain.

  • Dzeko kuondoka Man City

    Edin Dzeko

    Kocha Mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini amekubali kuwa mshambuliaji wake Edin Dzeko anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo.

    Dzeko mwenye miaka 19 yupo pamoja na kikosi cha Man City katika safari ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huko Australia na hakucheza wakati timu hiyo ilipocheza na AC Roma ya Italia siku ya jumanne.
    Kuna taarifa Dzeko huenda anaweza kuhamia kuchezea moja ya vilabu huko nchini Italia.

  • RASMI ARTURO VIDAL NI MCHEZAJI WA BAYERN MUNICH


    C.E.O wa Bayern Munich ame-conferm kuhusu usajili wa Vidal kujiunga na club yao leo hii. Karl-Heinz Rummenigge ametoa taarifa rasmi kwa vyombo habari kuhusu uhamisho huo.
    “Ninaweza kuthibitisha kwamba kimsingi tumefanikiwa kufikia muafaka kati yetu na Juventus pamoja na Vidal. Kilichobaki ni kupitia vipimo vya afya na kusaini mkataba wenyewe. Tunategemea mambo yataenda vizuri na haraka ili ajiunge na mazoezi ya club wiki ijayo”.
    Vidal ameisaidia club yake ya Juventus kucheza hadi fainali ya UEFA na pia timu yake ya taifa kuchukua kombe la Copa America.
  • Benteke ahamia rasmi Liverpool


    Timu ya livepool imekamilisha kumsajili rasmi mshambuliaji mwenye asili ya Jamuhuri ya Kidemokrasia wa kongo Christian Benteke kutoka Aston Villa kwa kitita paundi milion 32.5.

    Benteke alikubali mkataba wa muda mrefu na kuwa mchezaji wa pili kununuliwa kwa gharama kubwa huko England.

    Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ameifunga magoli 49 katika mechi 101 alizocheza kwenye timu yake ya zamani ya Aston Villa.

  • Jordon Ibe kusaini mkataba mpya Liverpool

    JORDON Ibe yuko mbioni kusaini mkataba wa muda mrefu baada ya Brendan Rodgers kuamua kuingiza vijana kwenye kikosi cha msimu ujao.
     
    Liverpool walimpa Ibe ofa ya mkataba mfupi mwezi februari baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mechi za ligi hususani dhidi ya Everton na Tottenham.
     
    Dili hilo sasa limeshafikiwa makubaliano na Ibe ambaye amekosekana tangu apate majeruhi ya goti dhidi ya Besiktas februari 26
  • Walcott na Sterling kubadilishana timu

    Jarida la Starsport limebainisha kuwa Liverpool na Arsenal zinapanga makubaliano ambayo yatazifanya timu hizo mbili kubadilishana wachezaji wawili wa taifa la Uingereza.

    Liverpool inahitaji pauni millioni 20 kwa nyota wake Sterling pamoja na mchezaji wa Arsenal Theo Walcot kwa mpango huo kukubalika.

    Walcott angejiunga na Liverpool msimu uliopita iwapo Luis Suarez angejiunga na Arsenal.
    Sterling

    Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa tayari kumuachilia Walcott kujiunga na Liverpool lakini Suarez akabadili nia na kujiunga na Barcelona.

    Sasa mpango kama huo umeanza kuandaliwa huku Sterling mwenye umri wa miaka 20 akipendelea kujiunga na Arsenal naye Walcott akikosa fursa ya kuanzishwa katika kilabu ya Arsenal.
  • David De Gea mikononi mwa Real Madrid? Pata majibu hapa

    Klabu ya Real Madrid imeweka mpango wa kumsajili kipa wa kimataifa wa Hispania David De Gea ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Manchester United ya England.

    De Gea kwa muda mrefu ametajwa katika mipango ya usajili ya Real Madrid lakini kwa sasa Madrid wanaonekana kuthibitisha kile ambacho kimezungumzwa na vyombo vya habari barani ulaya .

    Magazeti Uingereza hayajapitwa na hii story, yameandika kwamba Bodi ya Real Madrid imekaa na kujadili usajili wa kipa huyu ambapo imesemekana kuwa klabu hii inajiandaa kupeleka ofa ya kwanza kwa United na imejiandaa kupokea majibu ya hapana!
    Real Madrid inajiandaa kumbadili kipa wake wa muda mrefu Iker Cassillas ambaye kwa sasa anaonekana kushuka kiwango.Real Madrid inajiandaa kumbadili kipa wake wa muda mrefu Iker Cassillas ambaye kwa sasa anaonekana kushuka kiwango.

    Madrid imesema kuwa haitakuwa tayari kulipa fedha nyingi kuliko kawaida endapo United itataka fedha nyingi na badala yake wanajindaa kumsubiri De Gea hadi hapo mkataba wake utakapomalizika ili kumsajili bila gharama yoyote.

    Endapo haitampata De Gea Real Madrid imejipanga kuzungumza na Chelsea juu ya usajili wa kipa raia wa jamhuri ya Czech, Petr Cech ambaye klabu hiyo ya London imemuweka sokoni kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.

    Real Madrid inamtazama  De Gea kama mrithi wa muda mrefu wa kipa namba moja wa Hispania, Iker Cassillas ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akicheza chini ya kiwango mpaka kulaumiwa na watu wengi.
  • Beki matata Danilo atua Real Madrid

    Klabu ya Real Madrid imethibitisha kumsajili beki wa kulia wa klabu ya Porto Danilo Da Silva kwa ada ya euro milion 31.5 kwa mkataba wa miaka 6.

    Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa akisakwa na klabu za Arsenal,Chelsea na Bayern atajiunga na mabingwa hao wa ulaya baada ya msimu huu kumalizika

    Beki huyo alijiunga na wababe hao wa ureno mwaka 2012 na msimu huu ameisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.

    Aidha Danilo alicheza mechi yake kwanza katika timu ya taifa ya Brazil mwaka 2011 na pia ameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mechi ya kirafiki waliyocheza dhidi ya Chile jumapili iliyopita.
  • SAFARI YA GERRARD KWENDA MAREKANI YAIVA..

    Steven Gerrard akishangilia baada ya kufunga goli katika ushindi wa Liverpool wa mabao 3-2 dhidi ya Tottenham jumanne iliyopita

    Steven Gerrard atakutana na mabosi wa LA Galaxy kwa mara ya kwanza wiki hii.


    Nahodha huyo wa Liverpool anayeondoka Anfield anakutana na mabos
    i hao ana kwa ana kuzungumzia suala lake la kujiunga na klabu hiyo ya Marekani mwezi julai mwaka huu.
  • Southampton yasajili mchezaji wa pili Afrika Mashariki

    Baada ya kumsajili Mkenya Victor Wanyama, Southampton FC ya Ligi Kuu ya England (EPL), imesajili mchezaji wa pili kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili na nusu Mganda Bevis Kristofer Kizito Mugabi.

    Hata hivyo, beki huyo ambaye wazazi wake wote wawili ni Uganda, ana uraia wa nchi mbili unaomruhusu kuichezea timu ya taifa ya Uganda (Cranes) kwakuwa bado hajacheza katika kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa ya England.

    Mchezaji huyo amekaririwa katika mtandao rasmi wa klabu Southampton FC akisema amefurahi kupewa nafasi ya kukipiga katika klabu hiyo baada ya kuachwa huru na Fulham U18 Julai 2011. Amesema ana matumaini ya kufanya vizuri kwa kujituma kazini.

    “Nimefurahi kupata nafasi hii, nimesaini na kila kitu kimekamilika. Lengo langu ni kucheza katika kikosi cha kwanza. Nitafanya kazi kwa bidii mazoezini na wakati wa mechi,” amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 19.

    “Klabu imenipa nafasi baada ya Fulham kuniacha niende zangu. Hii ni sehemu nzuri kwa mchezaji mchanga. Southampton imetoa wachezaji wakubwa na ninaamini nitakuwa mmoja wao,” amesema zaidi.

    England U17

    Beki huyo wa kati aliitwa kwa mara ya kwanza katika vikosi viwili vya England U17 lakini hakufanya vyema kutokana na majerha ya goti, amekichezea kikosi cha Fulham mechi nane akifunga mabao matatu yakiwamo mawili katika mechi mbili dhidi ya two Chelsea na Everton.

    Anaungana na Jordan Turnbull na Jason McCarthy ambao wote wiki hii wametia saini ya kukipiga katika kikosi cha Martin Hunter cha U21 kabla ya kupelekwa Kikosi A cha Ronald Koeman.
  • ROMELU LUKAKU AWINDWA NA WEST HAM, TOTTENHAM

    Romelu Lukaku anaweza kuondoka Goodison 
    KLABU za West Ham na Tottenham zimeanza mipango ya kumshawishi mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku ili kuinasa saini yake majira ya kiangazi mwaka huu.
     
    Wiki iliyopita Lukaku alisema yuko tayari kuondoka Goodison ikiwa ni msimu mmoja tu tangu asajiliwe kwa paundi milioni 28 majira ya kiangazi kutokea Chelsea.
     
    Nyota huyo alisema kama itawezekana anaweza kurudi hata Chelsea, lakini haitatokea.
  • LUKAKU; Ntaka kuhamia klabu Kubwa

    Romelu Lukaku amesema ana matumaini ya kuondoka Everton kwa ajili ya "klabu juu" chini ya mwaka baada ya majira yake kubadili kudumu.

    Everton kuvunja rekodi ya uhamisho yao wakati wao kulipwa Chelsea £ 28m kwa ajili ya Ubelgiji mshambuliaji katika majira ya joto uhamisho dirisha.

    21 mwenye umri -old ilikuwa na mafanikio makubwa kwa mkopo katika Goodison Park kutoka Blues katika msimu wa 2013-14 lakini imejitahidi kurudia aina kwamba mwaka huu, ingawa yeye bado alifunga mara 10 katika mechi 36.

    Yeye alicheza dakika 90 ya Everton ya 1 -0 kushindwa katika Stamford Bridge Jumatano usiku, ambapo alikuwa radhi na mapokezi alipata kutoka kwa mashabiki nyumbani na pia alizungumzia nia yake ya kuendelea na mambo makubwa.

     "Ilikuwa kipaji kucheza katika Chelsea na mimi alikuwa mapokezi mazuri , "Lukaku aliiambia Sun. "Wanajua mimi nina mchezaji mzuri lakini kuwa nataka kuendeleza hivyo siwezi hatimaye kupata nyuma kucheza kwa klabu kama Chelsea.
    "Sina tamaa siri ili kujiunga - kuna klabu nyingine duniani. Mimi nataka tu kukua kama mchezaji na hatimaye kufika katika klabu ya juu tena. "
  • Tetesi za usajili Kwa ujumla: De Gea Ataondoka soma zaidi- THIS IS HABARI ?

    De Gea                     
    Mustakabali wa kipa David de Gea kusalia Manchester United upo shakani baada ya wakala wake Jorge Mendes kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa kumsajili.

    Manchester United inajianda kutoa ofa kwa timu ya Villarreal ili kumpata kumpata beki Gabriel Paulista, raia wa Brazil ambae yuko kwenye mazungumzo na Arsenal.

    Klabu ya Chelsea iko katika mipango ya kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.

    Bosi wa West Brom Tony Pulis imethibitisha kuhitaji kuwasajili winga wa Wigan Callum McManaman na kiungo Darren Fletcher toka Man United katika dirisha hili la usajili.

    Timu ya QPR imetoa ofa ya kumsajili mshambuliji wa zamani Ac Milan Alexandre Pato,anayechezea timu ya Sao paul kwa mkopo.

    Meneja wa Swansea City Garry Monk anavutiwa na mpango wa kumsajilibeki wa kushoto wa Norwich Martin Olsson, mwenye miaka 26,pamoja na kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart
    Kipa wa Manchester United David da Gea

    Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia winga wake Raheem Sterling, atasaini mkataba wa muda mrefu kusalia klabu hapo siku chache zijazo.

    Manchester City wameulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji Jay Rodriguez wa timu ya Southampton.

    Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham timu Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart Lane kwa kukosa namba kikosi cha kwanza.

    Kiungo wa zamani wa Chelsea Kevin de Bruyne,amekata kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi kurudi katika ligi pamoja na kwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester United.

    Klabu ya Roma inajaribu kiwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.
  • ARSENAL YAANZA MAKEKE YA USAJILI

    Klabu ya arsenal tayari imeanza mazungumzo rasmi ya kumuwania Kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan huku kiasi ya Pauni 16M zikitajwa kuhitajika katika usajili huo.

    Arsenal wamekuwa na tatizo la kiungo mkabaji kwa muda sasa tangu kuondoka kwa Alex Song aliyetimkia Barcelona na nafasi hiyo kucheza na Aaron Ramsey, Mikel Arteta na Methew Flamin huku wote wakionekana kupwaya.

    Pamoja na kufanya mazungumzo ya kumnasa kiungo huyo, Gunners wametajwa pia na magazeti ya leo barani Ulaya kumuhitaji mshambuliaji wa klabu ya PSG, Ednison Cavani ambaye anaonekana kuto ridhika na namna mambo yanavyoendelea kwa mabingwa hao wa Ufaransa.

     Kumpata Cavani kutaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Arsenal inayoongozwa na Alexies Sanchez ambaye amefunga magoli 10 ya ligi kuu mpaka sasa.

    Kwa upande mwingine, Arsenal wanaonekana kumuwinda kipa wa Chelsea Peter Cech na kula dalili za kumpata baada ya msimu huu kumalizika.

    Arsenal kwa sasa wanakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama 33 na wikendi hii watakuwa dimbani Emirates kuvaana na Stoke City majira ya saa 10:30 Jioni.

  • Usajili: Manchester United yaanza mazungumzo na PSG kumsajili Marquinhos

    Miezi 18 iliyopita PSG walitumia kiasi cha  €31.4m kwa ajili ya kumsajili beki wa kati wa AS Roma  Marquinhos.

    Mbrazil huyo mwenye umri miaka 20 amefeli kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Laurent Blanc na sasa yupo radhi kuondoka jijini katika dirisha hili la usajili la mwezi January.

    Vyombo vya habari vya Ufaransa likiwemo jarida linaloheshimika nchini humo Le 10 Sport limeripoti kwamba Manchester United wamewasiliana na PSG juu ya uhamisho wa Marquinhos lakini inawezekana uhamisho huo ukafanyika wakati dirisha lijalo la usajili.

    Marquinhos amekosa nafasi kwenye timu hiyo – huku wabrazil wenzie Thiago Silva na David Luiz wakichukua nafasi za kati kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.
    Louis Van Gaal ameripotiwa kuweka nguvu katika kumsajili beki wa kati mwezi huu na Marquinhos anatajwa ndio lengo lake.
  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.