Mecky Mexime
Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amesema timu yake haitauza wala kununua mchezaji yeyote mpya kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo.
Amedai kuwa hadi sasa wamerizika na wachezaji waliokuwa nao, na hakuna mapungufu ya ila kuimarisha mfumo tu.
Maxime ameiambia Goal, anajivunia mchanganyiko wa wachezaji aliokuwa nao kwenye kikosi chake ambao umekuwa na ushirikiano mkubwa na kuiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo katika mechi tisa za ligi ya Vodacom, walizocheza tangu kuanza kwa msimu huu.
“Hatutauza mchezaji kutoka kwenye timu yetu hivi sasa kwasababu ya kuhofia kuvuruga maelewana ya kiuchezaji yaliyopo kwa wachezaji wangu nilioanza nao msimu, nataka kuendelea na hawa niliokuwa nao ili kubakisha kasi yetu ambayo tumeanza nayo msimu huu,”amesema Maxime.
Maxime aliyeanza vizuri kuifundisha timu hiyo ndiyo kocha pekee mzawa ambaye yupo kwenye tatu bora na kumshinda Dylan Kerr wa Simba raia wa Uingereza ambaye timu yake inashika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 21.