![]() |
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe |
Prof Maghembe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mahojiano na kituo cha Redio One katika kipindi cha Kumepambazuka na kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi leo.
Alisema kazi ya kuuganisha bomba hilo ambalo litaongeza maji kutoka lita za ujazo milioni 180 hadi milioni 270, ilianza Ijumaa ya wiki iliyopita na ilitarajia kukamilika Jumapili, lakini ilishindikana kutokana na kukatika kwa umeme.
“Niahidi baada maji kutopatikana kwa siku kadhaa, sasa yataanza kutoka leo (jana) saa 11 jioni, mafundi watakuwa wameshakamilisha kazi ya kuunganisha hayo mabomba,” alisema Prof. Maghembe.
Alisema serikali imejipanga kuhakikisha ifikapo mwisho wa mwezi huu maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam yaanze kupata maji.
“Utandazaji wa mabomba umekamilika wa asilimia 90, kazi iliyobaki kuuganisha mabomba, ambayo tunatarajia kuwa yatakamilika ifikapo mwisho wa mwezi huu na maji yataanza kuingia kwenye matenki na hivyo maji yataanza kutoka katika maeneo mengi ya Jiji,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment