• Serenkuma wa Gor Mahia ajiunga na kilabu ya Simba

    Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu hiyo na kujiunga na Simba SC
     Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu  Simba SC.

    Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.

    ''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

    ''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
    Dan Sserenkuma
    Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katikamtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasaanatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjiniDaresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi

    Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
    Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.

    Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.