• UEFA CHAMPIONS LEAGUE: AS ROMA 0 vs 2 MANCHESTER CITY, SAMIR NASRI na ZABALETA WAIPA USHINDI CITY!


    Samir Nasri akishangilia bao lake la kwanza dakika ya 60 kipindi cha kwanza baada ya kumaliza kipindi cha kwanza bila bao.
    Dakika ya 60 Samir Nasri aliachia shuti kali lililogonga posti na kuzama ndani ya nyavu na kuipa bao City 1-0 dhidi ya As Roma kwenye Uwanja wao Stadio Olimpico, Roma Mwamuzi akiwa ni M. Mažić baada ya kupata pasi kutoka kwa Gael Clichy. Bao hilo lilifanya As Roma sasa waweze kutafuta bao mbili tena. 

    Bao la pili la Man City lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 86 na Pablo Zabaleta baada ya kupewa pasi na Samir Nasri.

    Dzekp akijaribu kuwatoka mabeki wa Roma

    Mabingwa wa England, Manchester City, watatinga kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi E la UEFA CHAMPIONS Ugenini huko Mjini Rome, Italy kucheza na AS Roma wakihitaji kushinda na pia miujiza mingine ili wafuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
    Kwenye Kundi E tayari Bayern Munich wameshafuzu na kuacha kinyang’anyiro cha Timu ipi itaungana nayo kwa Timu 3 zilizobakia ambazo ni AS Roma, Man City na CSKA Moscow.
    Timu zote hizo 3 zina Pointi 5 kila mmoja lakini nani ataungana na Bayern ni kitendawili kikubwa hasa ukichukulia Kanuni za UEFA hupima matokeo ya Uso kwa Uso kwa Timu zilizofungana Pointi.
    Kati ya Timu hizo 3 hatima ya AS Roma iko mikononi mwao wenyewe kwani wakiifunga City wao watafuzu.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.