• Wadai walifungwa kizazi na serikali Kenya

    Baadhi ya wanawake wanaodai kuwa walifungwa kizazi kwa lazima kutokana na hali yao ya HIV                

     Kikundi cha wanawake wenye virusi vya HIV nchini Kenya, kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali kikiituhumu kwa kuwapangaia wafungwe kizazi kwa lazima kutokana na hali yao ya HIV.

    Kwa mara ya kwanza katika historia ya kenya, kundi la kina mama ambalo lilikuwa limepokea kile serikali inadai kuwa msaada na ushauri wa afya, limejitokeza na kuwasilisha keshi mahakamani dhidi ya serikali, ikidai kuwa wao walishurutishwa kufunga uzazi na wengine baadhi yao wakifanyiwa upasuaji huo hata bila ufahamu wao.

    Akina mama hao ambao wanaishi na virusi vya HIV wanasema mpango huo unaoendeshwa na serikali kupitia wizara ya afya na mashirika mengine unakiuka katiba ya nchi na sasa wanataka kulipwa fidia na pia serikali kuharamisha mpango huo mbali na kuweka sera mpya kuhusu mpango wa kufunga uzazi.
    Wanawake hao wanataka serikali iwalipe fidia kwa oparesheni walizofanyiwa kinyume na matakwa yao

    Allan Malechi, ambaye ni wakili wao, anasema kuwa idadi ya wanawake hao waliofanyiwa upasuaji wa kufunga uzazi bila idhini yao huenda ikaongezeka zaidi kwa kuwa kuna ripoti kuwa mradi huo unaendelea katika sehemu zingine.

    Mashirika ya kutetea haki za kijamii pia yalijiunga na kina mama hao kwa maandamano ya amani mjini Nairobi.

    Wakiwa wamevalia mavazi yenya maandishi , ''koma mpango wa kulazimisha kina mama wanaoishi na virusi vya ukimwi, kufunga uzazi, '' wanaharakati hao wamesema kuwa mradi huo ni sawa na ukatili wa kibinadam na kutaka serikali kuptia kwa wizara ya afya kutoa taarifa rasmi.

    Inviolata Mwali ni mshirikishi wa kimataifa wa shirika la wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi Kenya.

    Wanawake hao wanataka kulipwa fidia na serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyowafanyia operesheni hizo.

    Pia wametoa wito kwa serikali operesheni kama hizo zikomeshwe.

    Kesi kama hizi zimewahi kuwasilishwa mahakamani katika mataifa kadhaa ya Afrika.

    Mahakama nchini Botswana mnamo mwaka 2012, iliamua kuwa wanawake watatu wanaoishi na virusi vya HIV waliofungwa kizazi kwa kulazimishwa walipwe fidia na serikali.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.