Afisaa mmoja mkuu (Joaquim do Espirito Santo) anasema kuwa mkutano wa kikanda uliotarajiwa kufanyika leo, umefutiliwa mbali kwa sababu ya hofu ya kuchelewesha mipango ya kijeshi dhidi ya waasi hao.
Umoja wa mataifa ulithibitisha mwishoni mwa wiki jana kwamba waasi wa FDLR wamepitwa na muda waliowekewa wa mwisho kwao kusalimisha silaha.
Wiki jana Rais wa DRC, Joseph Kabila, aliambia katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupambana na waasi hao.
Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa, (Martin Kobler) amesema kuwa hatua za kijeshi ndizo pekee zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya waasi ha
o kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment