Morocco imepinga kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kugoma kuwa mwenyeji wa Fainali za 2015 za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuhofia mlipuko wa Ebola.
Baada ya kufungiwa kwa nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika, Shirikisho la Soka la Morocco limepinga vikali adhabu hiyo likidai ni ‘ya kushangaza’.
Mwishoni mwa mwaka jana, nchi hiyo ilitaka kusogezwa mbele kwa michuano hiyo kutokana na hofu ya mlipuko wa Ebola kutoka na mashindano hayo kuvuta hisia za watu wengi, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Morocco.
Equatorial Guinea iliingilia kati na kuomba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na ilifanikiwa, licha ya kuibuka kwa vurugu zilizoharibu mechi ya nusu fainali kati ya wenyeji na Ghana.
CAF ilithibitisha mapema mwezi huu kuwa Morocco itafungiwa kushiriki Afcon mbili zijazo wakati pia ikitozwa faini ya dola za Marekani milioni moja huku pia ikilazimishwa kulipa fidia ya kuharibu mipango €8.5m.
Baada ya kikao cha Kamati ya Wakurugenzi ya Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) jana Jumanne, imeelezwa kuwa wameshangazwa na uamuzi huo na wanapinga kufungiwa.
“Kikao cha Kamati ya Wakurugenzi kimeeleza kusikitishwa na uamuzi huo mgumu na mkubwa wa CAF,” inasomeka taarifa katika mtandao rasmi wa FRMF.
“Kamati ya Wakugenzi wa FRMF inapinga uamuzi wa kufungiwa na kufungiwa kwa misaada ya kifedha, na inaona kuwa maamuzi hayo yaliyochukuliwa na Kamati ya Utendaji ya CAF yanarudisha nyuma maaendeleo ya soka la Afrika, na hayajazingatia kanuni yoyote.”
0 comments:
Post a Comment