Kauli hiyo ilimechukuliwa kama changamoto kubwa Italia ambako kumeshuhudiwa kupungua kwa uzazi kwa kiwango kikubwa hivi sasa.
Papa amesema jamii iliyoko katika kizazi kisichotaka kuzungukwa na watoto, kinachowachukulia watoto kama chanzo cha shaka na matatizo ni jamii iliyokubwa na msongo wa mawazo, kwani kuchagua kuto kuwa na watoto ni ubinafsi, maisha huwa mazuri na kupata nguvu mpya kizazi kinapoongezeka.
Papa alionya utamaduni wa maisha bora yanayoweza kupatikana wakati wanandoa wanapokuwa hawana watoto, lakini wana fedha za kutosha na kusema inaonekana kuwa faraja ya kuwa na Mbwa, Paka na kuwaonyesha mapenzi wanyama hao jambo ambalo sio sawa na baadaye ndoa hiyo huishia kwenye uzee wenye uchungu na upweke mkubwa.
0 comments:
Post a Comment