Polisi
nchini Misri wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
waandamanaji wanaopinga hatua ya mahakama nchini humo kutupilia mbali
kesi ya mauaji dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.
Awali Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo kwa sasa anatumikia pia kifungo cha miaka mitatu kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa sasa Hosni Mubarack anashikiliwa katika hospitali ya jeshi ambako pia anapatiwa matibabu.
Waziri wake wa zamani wa mamabo ya ndani Habib al-Adly na wenzake sita walihukumiwa kifungo cha maisha 2012, inakadiriwa takriban watu 800 waliuawa wakati wa harakati za kumuondoa kiongozi huyo Februari 11.2011.
0 comments:
Post a Comment