![]() |
Viwanda vikitoa moshi angani na kuchafua mazingira |
Mwaka
huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto
duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Na miezi kumi na mmoja ya kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.
Utafiti mwingine uliofanywa na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu.
Shirika hilo limesema kupanda kwa viwango vya joto katika uso wa bahari vilikuwa vinasababisha mvua zisizo za kawaida katika nchi za Morocco, Uturuki na nchi za Blakan, Ulaya mashariki na kusababisha
ukame mkali katika maeneo mengine duniani.
Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Michel Jarraud, amesema kuongezeka kwa utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira na mgandamizo wake angani kunaisababishia dunia kutokuwa na uhakika wa hali ya hewa na hali mbaya ya baadaye.
0 comments:
Post a Comment