KAKA
wa Emmanuel Adebayor, Kola amesema kwamba mshambuliaji huyo amevurgwa
na imani na kiislamu kiasi cha kufikiria mama yao anawaloga ili
asing'are uwanjani.
Kola,
mwenye umri wa miaka 42, dereva wa lori mjini Bremen, Ujerumani,
ameiambia The Sun jana kwamba: "[Emmanuel] amevurugwa na Waislamu
wanaomuambia sababu za kufunga mabao na kwa nini hafanyi vizuri kwa sasa
akicheza.
Hivi
karibuni Adebayor alikanusha madai ya dada yake, Maggie kwamba
alimfukuza mama yao, Alice katika nyumba yao Afrika kwa sababu anafikiri
anamloga.
Dada
huyo huyo wa Ade Mabao aisema kwamba mama yao alikuwa anauza mifuko ya
nailoni na kufuli na vitu vingine kuilea familia yake, pamoja na hayo
Emmanuel akasema mama yao aliondoka nyumbani kwa sababu zake.
Adebayor,
akizungumza na kituo cha Redio cha Peace FM, amesema: "Sikuwahi
kumfukuza mama yangu nyumbani. Aliamua kuondoka mwenyewe. Nitawezaje
kuguswa na mama yangu ambaye anamuambia kila mmoja kazi yangu haitasionga mbele, hivyo lazima nitakuwa upande wangu na kufanya yangu,"amesema.
0 comments:
Post a Comment