• LIGI KUU ENGLAND CHELSEA WAENDELEZA KIPIGO, ALEXIS SANCHEZ AZIDI KUWA MSAADA MKUBWA KWA ARSENAL

    Alexis Sanchez ameifungia Arsenal mabao 8 kwenye EPL msimu huu.
    Ligi kuu ya England imeendelea usiku huu kwa michezo mine iliyozikutanisha timu nane za ligi hiyo .
    Kwenye uwanja wa Emirates , Arsenal waliweza kushinda mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kuwafunga Southampton 1-0 ukiwa ni ushindi wao wa pili mfululizo wakishinda kwa bao moja .
    Bao hilo lililowapa Arsenal ushindi lilifungwa na Alexis Sanchez ukiwa ushindi wa kwanza kwa Arsenal dhidi ya timu iliyoko kwenye nafasi za tatu bora .

    Kwingineko Chelsea walishinda mchezo wao dhidi ya Tottenham kwa matokeo ya   3-0 . Ushindi huo ulikuja baada ya mabao ya Edin Hazard , Didier Drogba na Loic Remy .

    Mshambuliaji Didier Drogba akifunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Tottenham.
    Edin Hazard akifunga bao la kwanza kwa chelsea.
    \


    Katika mchezo mwingine Hull City na Everton walitoka sare ya 1-1 , na Man city wakawafunga Sunderland 1-4 .
    Matokeo haya yanamaanisha kuwa Chelsea wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 33 wakiwa wamewazidi Man city kwa pointi sita , Southampton ambao leo hii wamepoteza mchezo wao wa pili mfululizo wamejikuta wakishuka zaidi huku tofauti yao na Man United inayoshika nafasi ya 4 ikiwa pointi moja pekee .

  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.