• Mchezaji mwenye Tattoo nyingi kuliko wote.


    Wacheza soka wamekuwa na kawaida ya kupenda Sanaa ya kuchora miili yao ambapo mpaka leo hii asilimia kubwa ya wachezaji hawa hasa wale wanaoonekana sehemu mbalimbali barani ulaya wakicheza soka la kulipwa wamekuwa wakionekana kuwa na tattoo.

    Michoro hii huwa inahusu vitu tofauti wengine huandika namba za jezi wanazovaa ambazo zimekuwa kama utambulisho wao huku wengine wakiwa wanachora sura za watu wao wa karibu kama vile mama zao , wake zao na watoto wao , wengine huandika kumbukumbu muhimu kama vile majina ya viwanja na tarehe za kuzaliwa na zile zinazokumbushia matukio waliyowahi kuyafanya .

    Hivi karibuni mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Carlos Tevez alichora tattoo ambayo yawezekana ikawa ndio tattoo kubwa kuliko zote ambazo zimewahi kuonekana .

    Tevez amechora tattoo ambayo imefunika mgongo wake wote ikionekana kama vile amevaa shati la rangi tofauti .

    tev


    Tatoo hii imeanzia mkononi mwake na imezunguka mgongo wote na baadhi ya maeneo ya mbele ya mwili wake .

    Hivi karibuni Tevez akitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter alimshukuru mchora tattoo wake kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuchora mgongo wake wote .
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.