Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi anayesifika kwa kuzisumbua timu zinazomsajili kwa kutorejeakambini mapema pindi anapopewa likizo,ameanzakuuchanganya uongozi wa Simbakutokana na kutorejea kwake nchini kujiandaakwa mechi ya ‘Nani Mtani Jembe 2 dhidi yaYanga.
MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi anayesifika kwa kuzisumbua timu zinazomsajili kwa kutorejeakambini mapema pindi anapopewa likizo,ameanzakuuchanganya uongozi wa Simbakutokana na kutorejea kwake nchini kujiandaakwa mechi ya ‘Nani Mtani Jembe 2 dhidi yaYanga.
Baada ya kusimama kwa Ligi Kuu ya VodacomTanzania Bara (VPL) msimu huu Novemba 9,Okwi na wachezaji wengine wa Simba walipewamapumziko ya wiki mbili lakini Mganda huyo hajarejea nchini kuungana na wachezaji wenzakekatika mazoezi yaliyoanza Jumatatu ya wikiiliyopita kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwakwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Desemba 13.“Okwi amechelewa kurejea nchini kwa sababu
aliomba ruhusa baada ya kukumbwa na matatizoya kifamilia akiwea kwao (Uganda) wiki iliyopita,”amesema msemaji wa Simba, Hamphrey Nyasiokatika mkutano na waandishi wa habari jijini jana.Lakini, mwanzoni mwa wiki Makamu wa Rais waSimba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema mchezajihuyo wa zamani wa Etoile du Sahel ya Ligi Kuuya Tunisia na Yanga, atachelewa kurejeaTanzania kwa vile anajiandaa kufunga ndoa.Okwi amekuwa na desturi ya kutorejea klabunikwake kipindi cha sikukuu za Krismas na mwaka
mpya, hasa Sikukuu ya Krismas ambayohuazimisha pia tarehe ya kuzaliwa kwake 1992.
Mganda huyo alijiunga na Simba dakika chachekabla ya dirisha la usajili msimu huu kufungwaAgosti 28 akiwakacha Yanga waliokuwawamechoshwa na utaratibu wake huo wakutorejea mapema kikosini apewapo likizo nakuamua kutomalizia fedha za usajili wake nakutomlipa mishahara.Baada ya kurejea Simba, Okwi aliahidi kuchezasoka kwa bidii akiwa na kikosi cha wanamsimbazina kuachana na tabia zake sizizofaa, lakiniinaonekanasomo halijamuingia vizuri.
Kikosi cha Simba kiko kambini kwenye moja yfukwe za Jiji la Dar es Salaam na leo jioni itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya The Epress ya LigiKuu ya Uganda kukijiandaa kwa mechi ya Nani Mtani Jembe 2.
Shafii dauda. Chanzo.
0 comments:
Post a Comment