Mshindi huyo wa tuzo za Grammy, alipanda kizimbani Alhamis hii kwenye mahakama ya Los Angeles nchini Marekani ili kusikiliza ripoti ya maendeleo ya probation hiyo.
Jaji alimkanya kwa kutumbuiza kwenye show ya hivi karibuni huko San Jose bila kupewa ruhusa ya kusafiri. Wakili wake Mark Geragos alimueleza jaji huyo kuwa ofisi yake ilimshauri vibaya Brown kuwa hakuhitaji ruhusa ya kusafiri.
Brown pia alikuwa anatakiwa kumaliza masaa 1,000 ya kazi za jamii mwishoni mwa January lakini bado amebakiza masaa 200. Ataendelea kuwa huru hadi March 20 ambapo kesi yake itasikilizwa tena na maofisa wa probation kusoma ripoti yao.
Anatarajia kuanza ziara yake na Trey Songz ‘Between the Sheets Tour; Jan. 28 huko Hampton, Va.
0 comments:
Post a Comment