• Madee: Sijamzungumzia Chidi Benz kwenye wimbo wangu mpya ‘Vuvula’

    Wimbo mpya wa Madee ‘Vuvula’ uliotoka wiki hii, umeibua hisia kwamba amemzungumzia Chidi Benz. Mstari uliosababisha watu kuhisi hivyo unasema “wewe mtoto wa Ilala acha ngada vuta sigara…” Maana ya ngada ni ‘unga’.
     Akizungumza na XXL ya Clouds Fm Madee amekanusha kumuimba Chidi ambaye pia anaishi Ilala.
    “Unajua labda kwasababu Chidi anaishi maeneo ya Ilala, so mi niliitumia Ilala kama center of Dar es salaam kunakaa vijana wengi kwahiyo na wimbi kubwa ambalo limetanda sasa hivi Dar es salaam nini, baadhi ya vijana wengi kutumia madawa ya kulevya especially wasanii. Sasa nani ambaye anaweza akawakemea wasanii au akawakemea vijana kama sio sisi wenyewe wanamuziki au sio sisi vijana wenzao, kwahiyo nilikuwa najaribu kuwakemea vijana wote ambao wanatumia madawa ya kulevya sema nimetumia neno Ilala kwasababu ni center ya Dar es salaam, nilishataja Manzese tayari kwenye nyimbo, nimetaja Kimara nimetaja Mwananyamala so nimetaja Ilala kama imekuwa tatizo, lakini sijamzunguzmia Chidi” alisema Madee.

    Rapper huyo wa Tip Top Connection pia ametoa maana ya ‘Vuvula’ kuwa ni mtu mshamba ambaye hajielewi.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.