Bao la Dusan Tadic wa Southampton liliinyima United pointi tatu na kuishusha toka nafasi ya tatu hadi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya England . |
Kuikosa michuano ya ligi ya mabingwa kunatarajiwa kuigharimu klabu hiyo kufuatia hasara ambayo imetabiriwa kuipata wakati wa kufunga mahesabu kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 jambo ambalo hata hivyo linaweza kuwa limetatuliwa na mikataba ambayo United imeingia na wadhamini kadhaa .
Hata hivyo hasara itakuwa kubwa zaidi endapo United itashindwa kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa kwa mara ya pili mfulululizo na hili ni jambo ambalo Mkurugenzi Mtendaji Ed Woodward wala asingependa hata kuliwaza .
United itapoteza kiasi cha paundi milioni 50 ambazo zinatokana na mapato ya mlangoni na fedha za ushiriki wa mashindano haya endapo hawatafuzu ligi ya mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na Ed Woodward mwenyewe alinukuliwa akithibitisha ukweli wa hili .
Kiasi hicho kitakuwa sehemu ya hasara ya paundi milioni 150 ambazo United itaziripoti kama hasara kutokana na kusajili wachezaji na gharama nyingine kama mishara ambazo kimsingi zitashindwa kurudi kutokana ligi ya mabingwa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato .
Zaidi ya hapo hatari kubwa pengine kuliko zote ni kipengele cha mkataba wa udhamini ambao timu hii iliingia na kampuni ya vifaa vya michezo ya adidas ambapo endapo United itashindwa kufuzu ligi ya mabingwa asilimia 30 ya thamani ya mkataba ilio nao na kampuni hiyo itapungua
United ilipoteza mchezo wake wa ligi ya England uliopigwa jana kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Southampton hali iliyosababisha timu hiyo kupitwa na kushuka mpaka nafasi ya nne na tofauti kati ya timu ya nne na timu ya sita na kushuka chini ni ndogo hali inayosababisha wasiwasi wa timu hii kukumbwa na marejeo ya msimu uliopita wakati iliposhindwa kufuzu ligi ya mabingwa baada ya kumaliza nafasi ya saba .
0 comments:
Post a Comment