Walioshuhudia makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.
Awali, Rais Abd Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu.
Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili hali nchini Yemen.
Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia sjirika la habari la AP kwamba waasi haowalivamia ikulu nyakti za mchana.
Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walioivamia ikulu.
0 comments:
Post a Comment