![]() |
Waandamana Burundi wakimuunga mkono mwandishi aliyeachiliwa kwa dhamana kwa tuhuma za mauaji |
Walioshuhudia wanasema kuwa yalikuwa maandamano makubwa kuwahi kufanyika katika mji huo kwa miaka kadhaa.
Bobo Rugurika anayekifanyia kazi kituo cha redio cha African Public Redio aliwachiliwa kwa dhamana.
Alishtakiwa mwezi uliopita kwa kuhusishwa na mauaji ya watawa watatu raia wa Italy baada ya kurusha mahojiano hewani na mtu anayedaiwa kuwa mmoja ya wauaji.
Mahojiano hayo yalihitilafiana na uchunguzi wa polisi kuhusu uhalifu huo na kumtuhumu afisa mmoja mwandamizi.
Kituo hicho cha redio kinaonekana kupendelea upinzani.
Chanzo; BBC
0 comments:
Post a Comment