Mshambuliaji Cristiano Ronaldo amekuwa miongoni mwa wafungaji watatu bora katika historia ya Real Madrid baada ya hapo jana kufunga goli lake la 290 tangu atua klabu hapo mwaka 2009 kwa ada ya paundi milioni 80 akitokea kunako klabuni ya Manchester United.
Ronaldo alifunga goli hilo katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Elche huku goli lingine la matajiri hao likifungwa na karim Benzema katika mchezo huo uliopigwa Estadio Manuel Martinez Varelo jana.
Mshindi huyo wa Ballon D’or mara tatu sasa ameifikia rekodi ya gwiji wa klabu hiyo Carlos Santillana ambaye alifunga magoli 290 katika mechi 645 alizoichezea Real Madrid lakini Ronaldo ametumia mechi 281 kufunga magoli hayo.
Ushindi huo wa jana unaifanya Real Madrid kuwa juu ya msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 4 na Barcelona ambao walichezea kichapo kutoka kwa Malaga katika mechi iliyopigwa juzi katika uwanja wao wa nyumbani Camp Nou.
0 comments:
Post a Comment