Juventus usiku huu wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa jumla ya mabao 5-1 dhidi ya Borussia Dortmund.
Waitaliano hao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 huku Nyota mwiba wa Juve pamoja na Argentina Carlos Tevez akianza kucheka na Nyavu katika dakika ya tatu kabla ya Morata kupachika bao la pili kunako dakika ya 70.
Kwa mara nyingine tena Tevez akawainua vitini mashabiki wa Juve kwa kutupia kambani bao la tatu katika dakika ya 80.

Kwa matokeo hayo Vibibi vizee hao wanakuwa wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya mchezo wa kwanza kushinda bao 2-1.
VIKOSI:
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Papastathopoulos, Subotic, Hummels, Schmelzer, Kampl, Bender, Gundogan, Reus, Mkhitaryan, Aubameyang.
Subs: Langerak, Kehl, Kagawa, Blaszczykowski, Kirch, Immobile, Ramos.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Vidal, Marchisio, Pogba, Tevez, Pereyra, Morata.
Subs: Storari, Ogbonna, Barzagli, Pepe, Padoin, Llorente, Matri.
0 comments:
Post a Comment