Viongozi wa dini nchini Tanzania wameaswa kutumia muda mwingi katika kutoa elimu kwa waumini wao waachene na matendo mbalimbali yasiyo mpendeza mungu.
Kauli hiyo leo imetolewa na mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya ilala bwana JEREMIAH MAKORERE aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya ilala katika hafla fupi iliyoandaliwa na taasisi ya kiislam ya AL-MARID kwa ajili ya utoaji wa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji maalumu wakiwemo walemavu ambapo amesema kuwa kama maeneo ya ibada yatatumika ipasavyo yanaweza kuwabadilisha wananchi wakawa na roho ya kumuogopa mungu.
Baadhi ya waliopata misaada hiyo wakichambua kuona bidhaa walizopatiwa
Bwana
MAKORERE amesema kuwa kumekuwa na matendo mengi ya ukiukwaji wa haki za
binadamu ambayo yanafanywa na watanzania wachache kutokana na kuwa mbali
na mungu ambapo amezitaka taasisi mbalimbali za kidini kuwa katika
mstari wa mbele katika kukemea hali hiyo.
Akitolea
mfano wa mauaji yanayoendelea kushika kasi nchini tanzania ya watu wenye
ulemavu wa ngozi amesema kuwa pamoja na jitihadi kubwa zinazoonyeshwa
na serikali ya tanzania katika kutoa elimu pamoja na kudhibiti bado
matendo hayo yanazidi kuongezeka kutokana na watu kutokuwa na hofu ya
mungu hivyo akazitaka taasisi za kidini zote kwa umoja wao kuungana
kuhakikisha kuwa hofu ya mungu inarejea mioyoni mwa watanzania ili
kukemea matendo ambayo yanaonyesha kuvuruga amani ya Tanzania.
Baadhi ya misaada ikiwa tayari kutolewa kwa walengwa
Akizungumza
na mtandao huu msemaji na muweka hazina wa taasisi hiyo SHEKH RAJAB
KATIMBA amesema kuwa tasasisi yao imekuwa na utamaduni wa kutoa misaaada
mara kwa mara katika makundi mbalimbali nchini ambapo kwa safari hii
wamefanyia jijini dare s salaam na baadhi ya vitu waliivyotoa kama
msaada ni pamoja na nguo,vyakula,vifaa vya wanafunzi vya shule,pamoja na
misaada mingine ya kibinadamu.
0 comments:
Post a Comment