• SIMBA YAZIDI KUPOTEA YAPIGWA 2-0 NA MBEYA CITY

    MATUMAINI ya Simba SC kurudi kwenye michuano ya Afrika mwakani, jana yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

    Matokeo hayo, yanaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 42 za mechi 22.  Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 46, baada ya kucheza mechi 21.(P.T)

    Mbeya City ilipata bao lake la kwanza dakika za majeruhi kipindi cha kwanza, mfungaji Paul Nonga aliyemalizia pasi ya Deus Kaseke iliyompita beki Mganda, Juuko Murusheed. Mbeya City wameifunga Simba SC mabao 2-0 Sokoine jana Katika mchezo huo, Simba SC ilipata pigo dakika ya 23, baada ya beki wake tegemeo, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda, Joseph Owino. Isihaka, beki anayeinukia vizuri aliumia baada ya kugongana na Peter Mapunda.

    Mbeya City ilipata bao lake pili dakika ya 69, mfungaji Peter Mwalyanzi, aliyemalizia krosi Nonga aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Simba jana.

    Kikosi cha Mbeya City kilikuwa:

    Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Christian Sembuli, Juma Nyoso, Kenny Ally, Peter Mapunda/Hassan Kibopile dk77, Raphael Daud, Paul Nonga, Cossmas Freddy/Peter Mwalyanzi dk59 na Deus Kaseke.

    Simba SC:

    Peter Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Juuko Murusheed, Hassan Isihaka/Joseph Owino dk23, Abdi Banda, Jonas Mkude, Elias Maguli/Issa Abdallah dk56, Ibrahim Hajibu, Said Ndemla na Ramadhani Singano ‘Messi’.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.