Linahesabika kama tukio jingine la Basi
kuwaka moto katika rekodi za mabasi yaliyowaka moto yakiwa safarini
nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa
Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu baada ya kuongea na Mtandao wa
millardayo ni kwamba basi hili la kampuni ya Dar Express liliwaka moto
likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa
abiria.
Amesema ‘Ni kweli basi la Dar
Express saa saba mchana kwenye kijiji ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Pwani
lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote
wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima,
hakuna yeyote aliejeruhiwa‘
0 comments:
Post a Comment