Hapo Jumanne Mawaziri hao walikataa kutoa fedha za kuukwamua uchumi wa Ugiriki baada ya mazungumzo kuvunjika.
Ugiriki imekuwa nchi ya kwanza katika Muungano wa Ulaya kushindwa kulipa deni lake kwa IMF. Msukosuko wa sasa wa kifedha imezua hofu huenda Athens ikalazimika kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Mkutano wa Jumatano utaamua ikiwa Ugiriki itapokea mkopo wa dharura. Aidha Ugiriki pia imeomba kupewa fedha zaidi kuuchepua uchumi wake.
Katika kipindi cha miaka miwili Ugiriki imepokea Euro bilioni 29.1. Mmoja wa washauri wakuu wa serikali ya Ugiriki Elena Panaritis, ameambia BBC wanatarajia kupata msaada wa fedha waliopendekeza kupewa
0 comments:
Post a Comment