Shirika la afya duniani WHO, limesifia matokeo ya chanjo mpya ugonjwa wa Ebola, ambayo inatoa asilimia 100% ya kinga baada ya majaribio yake nchini Guinea.
WHO linasema kuwa ulimwengu unakaribia zaidi kupata chanjo mpya dhidi ya ugonjwa huo hatari wa Ebola.
Dawa ya chanjo hiyo ilijaribiwa maelfu ya watu, mara tu mtu mmoja aliyekuwa karibu nao alipoambukizwa ugonjwa huo, lakini baada ya kutibiwa kwa siku kumi hakuna hata mmoja wao alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 11,00 wamefariki kutokana na Ebola
Licha ya kuwa chanjo hiyo bado haijaidhinishwa rasmi ama kupewa leseni, tayari maandalizi yanafaywa ili isambazwe wa kote Duniani.
Zaidi ya watu elfu kumi na moja wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa ebola, tangu ilipolipuka nchini Guinea mwezi Disemba mwaka 2013.
Chanzo; BBC
0 comments:
Post a Comment