Agizo hilo lilikiuka kanuni za hospitali kwani watu wanaotangazwa kufariki hutakiwa kukaa kwenye wadi saa mbili, kuhakikisha hakuna kosa na ni kweli wamefariki dunia. Madaktari wanasema mwanamume huyo kwa jina Prakash alikuwa na matatizo ya mwili kuendesha shughuli za kawaida na alikuwa akiropokwa alipofikishwa hospitalini.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema alipatikana katika kituo cha mabasi akiwa amepoteza fahamu. Akiongea katika kikao cha wanahabari Jumatatu, Dkt Suleman Merchant, anayesimamia hospitali ya Lokmanya Tilak alisema Prakash ni mlevi “aliyejitelekeza” na alikuwa na mabuu usoni na masikioni.
"Miili ya wafu kawaida ndiyo huwa na mabuu. Lazima alikuwa amekaa pahali amelala siku sita au saba,” alisema daktari Merchant. Aliambia wanahabari kwamba daktari aliyemchunguza Prakash alimpima mpigo wa moyo, mpigo wa damu na hata kupumua kwake. Dkt Merchant amesema hospitali hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho. Prakash yuko katika hali thabiti hospitalini ambako anaendelea kutibiwa.
0 comments:
Post a Comment