• Leo mambo yatakuwaje pale Old Trafford Manchester United dhidi ya Manchester City Ligi Kuu ya Uingereza? Huu ni uchambuzi wa mechi

     
    Ikumbukwe mechi ya mwisho Man United walishinda 4-2 dhidi ya Man City, United walimiliki mpira kwa asilimia 58 bila kadi yoyote na kufanya faulo 9 tu wakati City walimiliki mpira kwa asilimia 42, kadi za manjano 3 na faulo 16, ishara kuwa City walizidiwa kila kona.

    Baada ya misimu miwili tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson na mchakamchaka wa miaka mingi, Manchester United watapata fursa ya kuimarisha utawala wao katika Manchester na katika Ligi Kuu ya Uingereza kwenye mechi ngumu dhidi ya Manchester City Jumapili.

    United watakuwa uwanja wa nyumbani Old Trafford wakishika nafasi ya tatu msimamo wa ligi, pointi mbili nyuma ya majirani zao na vinara wa ligi Man City.


    Litakuwa pambano muhimu kwa United katika jaribio lao kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi. Ni miaka mitatu sasa tangu walipotwaa ubingwa wa Ligi kwa mara ya mwisho ikiwa ni mara ya 20, na kipindi hiki ni mara yao ya kwanza kuonyesha ari ya kutaka tena kupata taji hilo.

    Ni baada ya muda usiozidi majuma matatu tangu United waliposalimu amri katika mechi mojawapo ngumu ya msimu. Dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates, Manchester United walijikuta wakitundikwa magoli mawili ya haraka ndani ya dakika saba na kuishia kichapo cha mabao 3-0 baada ya dakika 20 na kuhaha kuyarudisha bila mafanikio.

    Walizidiwa kila kona, sehemu ya kiungo na ulinzi zote zikiwa zimepwaya licha ya cheche za Anthony Martial kujaribu kuchochea mashambulizi.

    Changamoto kwa Van Gaal ni kuonyesha kiwango kikubwa katika mechi hii na kuhakikisha anapata ushindi katika mechi nyingine kubwa baada ya kudhalilishwa na Arsenal.

    Baada ya kipigo cha Arsenal, kocha huyo veterani wa kidachi aliwataka wachezaji wake kuamka kama, na walionyesha ushupavu kwa kuisambaratisha Everton bao 3-0.

    Pia United walionyesha kiwango kidogo sana katika mechi dhidi ya CSKA Moscow baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Ligi ya Mabingwa Jumatano usiku.

    Bado van Gaal anamuingiza Wayne Rooney katika wachezaji anaowategemea katika mechi hii kubwa kutokana na historia yake nzuri katika mechi ngumu za Manchester licha ya kuanza vibaya msimu huu kwa kushindwa kuonyesha uwezo wake wa awali.

    Manchester City watacheza mechi hii ngumu bila ya kipanga wao Sergio Agüero, ambaye anasumbuliwa na majeraha. Mkali mwingine wa Man City David Silva yu shakani kucheza mechi hii kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.


    Awali City walikuwa wakipata tabu wachezaji wake wakubwa wanapokosekana; kikosi chao licha ya utajiri mkubwa na ufahari, hakikuwa na mbinu za kutosha bila ya nyota wake. Lakini sasa baada ya kutumia euro milioni 100 kusajili washambuliaji wiwili majira ya joto kikosi kimeanza kuimarika hata bila ya Sergio Agüero.

    Katika mechi mbili zilizopita City walionyesha uwezo mkubwa. Jumamosi Raheem Sterling alipiga hat-trick kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kilipoibamiza Bournemouth 5-1. Siku nne baadaye, alikuwa mchezaji mwingine, Kevin de Bruyne, aliyeipaisha Man City baada ya kufunga goli safi na la kiufundi kuipa timu yake ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Chelsea ikiwa inazidi kudidimia, ni dhahiri Man City wana nafasi kubwa kunyanyua ubingwa wa Ligi ya Uingereza kwa mara ya tatu ndani ya misimu mitano katika kampeni hizi. Lakini pia kuna ishara nyingi za City kushindwa kujipatia ushindi mechi nyingi mfululizo.

    Vipigo kutoka kwa Juventus na West Ham pamoja na kile cha 4-1 dhidi ya Tottenham vinazidi kuipa Man United tumaini la kuifunga City.

    Utabiri: Sterling na De Bruyne watakuwa tishio kwa Man Utd, lakini kukosekana kwa Agüero, huenda na Silva, bado kunaifanya safu ya mashambulizi ya Man City kuwa dhaifu kwa kiasi fulani.

    Licha ya kuwa nyumbani, Van Gaal atahitaji kutumia akili nyingi na mbinu kuzuia mashambulizi ya Man City kwa kuweka wachezaji wenye uwezo wa kukaba, bila shaka Morgan Schneiderlin atahusika katika mechi hii.

    Safu ya ulinzi bado haiko thabiti, na inaweza kuvurugwa na ubora wa Man City. Lakini mwisho wa yote timu zote zinaweza kukubali kugawana pointi.

    Utabiri wa magoli: Manchester United 1-1 Manchester City
    Wachezaji majeruhi
    Manchester United: Luke Shaw na Paddy McNair wataendelea kuwa nje, wakati Ashley Young bado hakijaeleweka.

    Manchester City: Kama ilivyo kwa Agüero na Silva, Fabian Delph nao Gael Clichy wataikosa mechi hii.
    Kumbukumbu za mechi za awali na Wayne Rooney
    Wayne Rooney amefunga magoli 11 katika mechi kubwa za Manchester (michuano yote); akiwa amefunga magoli mengi kuliko mchezaji yeyote atakayeshiriki katika mechi hii kubwa itakayochezwa Jumapili.

    Rooney ana umri wa miaka 30 sasa – na hakuna mchezaji wa Ligi Kuu ya Uingereza aliyefanikiwa kufunga magoli mengi kama yeye katika umri wa miaka 30 (187)
    Manchester City wameshinda wameshinda mechi sita kati ya nane walizocheza dhidi ya Manchester United katika michuano ya Ligi ya Uingereza.

    Manchester United wameshinda mechi 17 kati ya 23 walizocheza wakiwa Old Trafford chini ya Louis van Gaal (74%), wakiwa wameruhusu magoli 16 tu (wamepoteza mechi 3 na kutoa sare 3)


  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.