Kikosi cha Simba kimewasili mkoani Mbeya tayari kwa ajili ya pambano la Jumamosi la Ligi ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbeya City pambano ambali litapigwa uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Msemaji wa Simba Haji Manara ameiambia Goal, wamekwenda mapema Mbeya kwa lengo la kuzoea hali ya hewa na mazingira ya sehemu hiyo ambayo inajulikana kuwa na baridi kali tofauti na Dar es Salaam.
“Tuna mechi mbili huku dhidi ya Mbeya City na baada ya hapo Jumatano tunacheza na Prisons ni mechi ngumu kwetu na tumepania kuchukua pointi zote sita ndiyo sababu tukaamua kuja mapema kwa ajili ya wachezaji waweze kuzoea hali ya hewa ili wasije kushindwa kumudu mchezo na kujikuta tunapoteza malengo yetu,”amesema.
Haji amesema kikosi chao chote kimekamilika ikiwemo wachezaji waliokuwa kwenye timu ya taifa na kwenye mchezo huo watamkosa beki wa kimataifa wa Burundi Emery Nimubona, aliyevunjika mfupa wa kidole na tayari amewekewa Plasta gumu.
0 comments:
Post a Comment