Kama utakumbuka mapenzi ya Chris Brown na Rihanna yalikuwa ya vituko kila siku. Mwaka 2009 mastaa hawa waliachana huku mwanamuziki Rihanna akibaki na majeraha mwilini kutokana na kichapo alichopta kutoka kwa Breezy. Lakini hawakuachia hapo bali miaka mitatu mbeleni walirudiana hadi pale Chris alipoachana na Rihanna na kuamuwa kuwa na Karrueche.
Kwakipindi hicho chote wawili hawa hawakuonekana pamoja hadi walipo kuja kukutana kwenye mixtape ya 'Fine By Me' yenye collaboration yao. Kwa Karrueche haikuwa kinyongo kwakuwa ameonekana aki share mixtape hiyo yenye ngoma 34 ikijumishwa na ngoma yao ya Chris Brown na Rihanna 'Counterfeit' ambayo imemsababisha Chris Brown atamani kuwa karibu masaa yote na Rihanna.
Kwamujibu wa HollywoodLife, Chris anataka kumualika Rihanna kwenye mchezo wa kikapu ambapo atakuwepo mkongwe wa game hilo anayetaka kustaafu kwa sasa michezo ya NBA Kobe Bryant. Mtu moja aliye karibu na Chris Brown amesema Chris na Kobe nimarafiki sana, Na Christmas itakuwa imekamilika kama Rihanna atakubali kujumuika “Kobe is one of Chris’ idols! Chris’ Christmas would be complete if Rihanna accepted the offer. Watching her smile and eat popcorn out the palm of his hands while watching Kobe play in his last season would be a dream come true for Breezy.”
Vipi kwa wewe shabiki wao, Ungependa Rihanna arudi kuwa na Chris Brown? Dondosha comment zako hapo chini.