Hayo yamedokezwa na Dkt. Nusaiba Ibrahim Zakzaky bintiye kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky. Akizungumza na Televisheni ya Press TV akiwa mjini Dubai,
Bi. Nusaiba alisema yamkini idadi ya waliouawa ikapindukia zaidi ya 1000.
Kuhusu sababu za kujiri mauaji hayo amesema baba yake amekuwa akitoa hotuba zenye muamko na yamkini jambo hilo limewakasirisha watawala wa Nigeria ambao wamekuwa wakiwakandamiza watu wa nchi hiyo. Siku ya Jumamaosi jeshi la Nigeria liliwafyatulia risasi Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa kwenye shughuli zao za kidini ambapo idadi kubwa ya waumini waliuawa.
Baadaye jeshi hilo lilivamia nyumba ya kiongozi mashuhuri wa kishia, Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuua idadi kubwa ya watu waliokuwa hapo kabla ya kumtia nguvuni.
Hadi sasa haijabainika aliko kiongozi huyo wa Kiislamu. Hapo jana Iran ilimuita balozi mdogo wa Nigeria mjini Tehran na kubainisha kustikitishwa kwake na mauaji ya Waislamu Nigeria.
Naye Hujjatul Islam wal Muslimin Mohsen Qumi, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha masikitiko yake kutokana na mauaji ya Mashia Nigeria na kusema serikali ya nchi hiyo inabeba dhima ya maisha ya Sheikh Zakzaky.
Chanzo: Radio Tehran