• KWANINI TUNAOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYE SAHIHI? JIBU HILI HAPA.

    1. Kwasababu ulitarajia atabadilika baadaye lakini imekuwa kinyume na matarajio yako.

    2. Kwasababu ulizingatia umbo na sio tabia wakati wa kuchagua mke au mume wa kuwa nae na mwisho wa siku mnagombana kutokana na kutokuendana kitabia.

    3. Kwasababu hujui nini mwenza wako anahitaji toka kwako. Kutokujua ni nini mwenza wako anahitaji itakuwa ngumu kuweza kuendana ndani ya nyumba.

    4. Kwasababu hamushirikishani malengo ya maisha na kila mtu anakuwa msiri na mwisho wa siku mnaishia kuona ndoa chungu.

    5. Kwasababu ya haraka ya kuoa au kuolewa pasipo kumjua mwenza wako vyema maadili yake na kama mtaendana ki tabia.

    6. Kwasababu umehitaji kuwa nae baada ya kuona ana mali nyingi kama magari na pesa na pasipo kuzingatia sifa zote na mume au mke wa kuoa au kuolewa nae.

    7. Kwasababu ya kusukumwa na mitazamo ya watu, wazazi kuchagulia watoto mke au mume ni tatizo kubwa sana.

    8. Kwa sababu hukumuweka wazi ni vitu gani unapenda na vitu gani hupendi. Na hatimaye mtaishia kugombana kutokana na kutokuelewana na kutoendana kimahitaji.

    9. Kwasababu uliingia kwenye mahusiano ili kuondoa upweke uliokuwa nao na ili kumaliza matatizo yako pasipo na utayari. Ndoa sio jawabu ya matatizo yako.

    10. Unakuwa na mtu mwenye maisha ya pembe tatu, yaani kuna kuwa na kitu cha ziada kimeingilia katikati ya mahusiano yenu na wewe hupewi kipaumbele sana.
    Chanzo:kumimuhimu
  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.