• Pistorius apatikana na hatia ya mauaji

    Pistorius aliondoka gerezani Oktoba mwaka huu
    Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini imempata mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius na hatia ya mauaji.

    Mahakama hiyo imekubali rufaa iliwasilishwa na upande wa mashtaka ikitaka Pistorius apatikane na hatia ya mauaji, ambayo adhabu yake ni kali zaidi kuliko ya kuua bila kukusudia.

    Jaji Lorimer Leach amesema mwanariadha huyo anafaa kurejeshwa kwa jaji aliyemhukumu ili apokee adhabu ya kosa la mauaji.

    Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi kupitia mlango wa choo.

    Amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia.

    Awali, ilikuwa imeripotiwa kimakosa kwamba rufaa hiyo ilikuwa imetupwa na angeendelea kutumia kifungo cha kuua bila kukusudia.

    Pistorius alifungwa jela miaka mitano mwaka 2014 baada ya kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia.
    Chanzo: BBC
  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.