• Treni ya mizigo yaanguka, abiria 1,000 wa treni wakwama Dodoma

    Zaidi ya abiria 1,000 waliokuwa wakisafiri kwa treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mikoani ya Kigoma na Mwanza wamekwama mkoani hapa baada ya treni ya mizigo kuanguka kati ya Kituo cha Itigi na Kitalaka.

    Akizungumza jana Mkuu wa Kituo hicho cha Dodoma, Suzo Kazimoto, alisema uongozi wa TRL, umelazimika kuzuia treni hiyo kuendelea kwa safari baada ya kupata taarifa za treni hiyo kuanguka katika eneo hilo.

    Alisema waliamua abiria hao wabaki mjini Dodoma ili wapate huduma zote muhimu za kijamii zinazopatikana kwa wingi tofauti na Itigi.

    Kazimoto alisema mafundi wako eneo la ajali wanaendelea na kazi ya kurejesha reli katika hali ya kawaida ili abiria hao waendelea na safari ya kwenda kwenye mikoa hiyo. “ Tumewatangazia abiria wetu kuwa safari yao itaendelea kuanzia saa 12:00 jioni leo (jana), alisema Kazimoto.

    Akijibu madai ya abiria kuhusu fedha za kujikimu, Kazimoto alisema wanakusanya tiketi halali na kuwasiliana na makao makuu ya kampuni hiyo ili kupata kibali cha kuwalipa fedha za kujikimu hadi watakapoendelea na safari.

    Aidha baadhi ya abiria walilalamikia uongozi wa TRL kwa kushindwa kujenga njia mbili tangu walipokabidhiwa reli hiyo na mkoloni kwani kama kungekuwa na njia mbili kama ilivyo katika nchi nyingine, safari yao ingendelea.

    Mmoja wa abiria hao, Khadija Salum aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea Kigoma, alilalamikia wahalifu kutumia mwanya huo kwa kumuibia Sh 70,000 kwa ajili ya kujikimu wakati wa safari. “Nao wafanyabiashara wametumia tatizo hili kujipatia faida kubwa kwa kupandisha bei ya bidhaa,” alisema.

    Read more at http://www.tubongetz.com/2015/12/habari_6.html#UlEPWXRw5dXdyuwu.99
  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.