January 30 Coiastal Union iliinyosha Yanga kwenye uwanja huo kwa bao 2-0 leo imefanikiwa kuilaza Azam FC kwenye uwanja huohuo kwa bao 1-0 lilifungwa na Miraji Adam dakika ya 68 kipindi cha pili kufatia makosa ya golikipa Aishi Manula ambaye aliundaka mpira na kubaki nao kwa madai alikuwa ameumia.
Mwamuzi akatoa adhabu (indirect free-kick) ya mpira upigwe eneo lilile ambalo Manula alikuwa amedaka mpira ndipo Adam Miraji akaipa Coastal bao la ushindi.
Baada ya Coastal Union kufanikiwa kuifunga Azam wamefanikiwa kuandika rekodi mpya kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara.
Costal ndiyo kiboko ya vigogo
Timu hiyo kongwe ya jijini Tanga imekuwa timu ya kwanza kuzimunga Yanga na Azam na kuzivunjia rekodi ya kutofungwa kwenye ligi msimu huu.
Ushindi ilioupata wa magoli 2-0 dhidi ya Yanga, ilikuwa ni mechi ya kwanza kupoteza tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Yanga walipoteza mchezo wao kwanza ikiwa ni raundi ya 15 ambayo ilikuwa ni mechi ya mwisho kukamilisha mzunguko wa kwanza.
Azam pia wameionja joto ya jiwe mbele ya Coastal Union ambayo imeivua rekodi ya kutopoteza mchezo kwenye ligi. Azam wamepigwa kwenye mechi yao ya 17 baada ya kucheza michezo 16 (raundi ya kwanza) bila kupoteza mchezo hata mmoja.