Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alisalia uwanjani na kupeana mkono na wachezaji wote wa Chelsea baada ya mchezo kumalizika.
Akiwa Chelsea mashabiki walimchagua mara mbili kuwa mchezaji bora wa mwaka. Mata bado anakumbukwa na kupendwa na mashabiki wa timu yake ya zamani hasa kutokana na nidhamu ambayo amekuwa akiionesha kwa wachezaji wenzake wa zamani kila anapokutana nao.
Mata aliondoka Stamford Bridge mwaka 2014 kutokana na ujio wa kocha wa zamani wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye hakuhitaji huduma ya mhispania huyo.
Lakini Mourinho pia yupo nje ya Chelsea, Mata ameonekana alikuwa mwenye furaha kukutana tena na wachezaji wenzake wa zamani.