• MAXIME ASEMA HAKUNA KULALA, NI USHINDI KWENDA MBELE

    Mtibwa Sugar leo itakuwa ugenini kukabiliana na Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  mkoani Mtwara katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

    Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime amesema kwamba wao wamejiandaa vyema na mchezo huo na watahakikisha wanapata matokeo ya ushindi ili kuendelea kujiweka vizuri kwenye msimamo au mazingira ya ligi kuu Tanzania bara.

    “Sisi tulishafanya maandalizi nyumbani, tumekuja kucheza na Ndanda tunajua ni timu nzuri ambayo imetoka kupata ushindi ugenini na watakuwa wanataka kupata ushindi wa nyumbani lakini sisi tumejiandaa kuja kupata pointi tatu”, amesema Maxime.

    Mtibwa Sugar ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 17 wakati Ndanda FC wao wanakamatia nafasi ya 11 kwa pointi zao 16.

    Mechi ya mwisho kabla ya mchezo wa leo Mtibwa ililazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Manungu Complex wakati Ndanda wao walishinda mchezo wa mwisho kwao bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya Coastal Union ya mkoani Tanga.

  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.