Kocha Manuel Pellegrini anasema Leicester wanabahati ya kusajili matokeo mema katika ligi ya Uingereza kwa sababu hawana mechi nyingi na pia hawashiriki mashindano tofauti kama wapinzani wao wakuu Arsenal .
Vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wamesalia na mechi 13 pekee msimu huu kwani wamekwisha banduliwa nje ya mashindano mengine.
Kwa upande wake vijana wa Pellegrini wamesalia na takriban mechi 27 katika kipindi hicho.
Manchester City inashiriki ligi 4 tofauti kwa wakati mmoja.
Man City inawania ligi ya mabingwa barani Ulaya , ligi kuu ya Uingereza , League Cup, na kombe la FA .
''Bila shaka ukilinganisha mahitaji yetu na idadi ya mechi tulizoratibiwa kucheza kufikia mwisho wa msimu ni zaidi ya mara mbili ya Leicester.''
''Kwa sasa wameelekeza bidii yao yote kwenye mechi hizi za ligi na hivyo wana muda bora wa kupumzika na kujiandaa kwa mechi ijayo'' alisema Pellegrini.
''laiti nas tungelikuwa tunajiandaa kwa mechi moja kwa wiki ,,,,bila shaka tungekuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kombe la ligi kuu''
Man City wameshuka hadi nafasi ya nne kufuatia kichapo hicho mikononi mwa Leicester ambao sasa wamefungua pengo la alama 5 zaidi ya washindi wa pili Tottenham.
Image copyright PA
Image caption Pellegrini amesalia na takriban mechi 27 huku Leicester wakisalia na mechi 13 pekee .
''Kwa sasa wachezaji wetu wanacheza mechi zaidi ya nne kwa juma na hiyo inasababisha majeraha mengi sana''
''Kwamfano vigogo wetu wa safu ya ulinzi Vincent Kompany na Eliaquim Mangala wamejeruhiwa ukitizama safu yetu ya mashambulizi hali ni mbaya zaidi Kevin de Bruyne, Jesus Navas, Wilfried Bony, Samir Nasri na David Silva wote wanauguza majeraha ni kizaza," Alisema Pellegrini.
''Hali ni Ngumu kwa kweli .Natumai tutapata nafuu karibuni''
Sasa Pellegrini anakabiliwa na ushindani zaidi kutoka kwa Tottenham Hotspurs siku ya jumapili.
Wikiendi ijayo itakuwa zamu ya Arsenal kuikaribisha Leicester uwanjani Emirati.