Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma ya kigaidi
dhidi ya msikiti katika mji Kano kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo
watu zaidi ya 120 waliuawa.
Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham amelezea masikitiko yake kutokana na kuenea ugaidi na misimamo mikali na kuongeza kuwa kuna haja ya hatua kuchukuliwa kuangamiza maovu hayo.
Aidha ametoa wito kwa Wanigeria kuungana na kuzuia njama ambazo zinaweza kuibua migawanyiko ya kimadhehebu na kikabika katika nchi hiyo. Kwingineko Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, naye pia amelaani vikali shambulizi la kigaidi kwenye Msikiti Mkuu wa Kano.
Ametoa wito kwa mamlaka za Nigeria ziwafikishie haraka waliotenda uhalifu huo mbele ya mkono wa sheria, akikariri kuwa hapawezi kuwepo kisingizio chochote kinachokubalika cha kufanya mashambulizi dhidi ya raia.
Ban ameahidi uungaji mkono kikamilifu wa Umoja wa Mataifa kwa juhudi za Nigeria za kupambana na ugaidi .
Ikumbukwe kuwa siku ya Ijumaa zaidi ya watu 120 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya watu 2 wanaoaminika kuwa wanachama wa Boko Haram kujilipua kwa mabomu ndani ya msikiti mkuu katika mji wenye Waislamu wengi wa Kano, kaskazini mwa Nigeria.
Magaidi hao wa kitakfiri waliingia msikitini humo wakati hotuba ya Sala ya Ijumaa ilipokuwa ikiendelea na kisha kujilipua.

0 comments:
Post a Comment