Klabu ya Liverpool huenda ikampoteza nahodha wake wa muda mrefu Steven Gerrad ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika .
Gerrad ambaye wikiendi hii ametimiza miaka 16 tangu alipocheza mchezo wa kwanza kwenye kikosi cha wakubwa cha klabu hiyo amekuwa kwenye mazungumzo ambayo hata hivyo hayajawa na amfanikio kuhusiana na kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo.
Kizingiti cha Gerard kuendelea kubaki kwenye timu kinaweza kuwa mshahara ambapo uongozi wa Liverpool uko tayari kumuongeza mkataba nahodha huyo ila kwa sharti la kupunguza nusu ya mshahara wake .
Gerard analipwa kiasi cha paundi za Uingereza 140,000 na uongozi wa Liverpool uko tayari kumlipa nusu ya mshahara huo ambayo ni paundi 70,000 .
Gerrard amekuwa mgumu kukubaliana na sharti hilo na kwa sababu hiyo huenda akalazimika kuondoka kwenda mahali kwingine ifikapo mwisho wa msimu huu .
Hali ya mkataba sio ngumu kwa Gerarrd pekee kwani hata beki mkongwe Glenn Johnson naye anakaribia kumaliza mkataba wake lakini uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa uko tayari kumuongeza mkataba ila shjarti ni lile la kupungua kwa nusu ya mshahara .
Yawezekana uongozi wa Liverpool unataka kuwekeza ka wachezaji wenye umri mdogo akiwemo mtu kama Raheem Sterling ambaye Liverpool inafanya naye mazungumzo ya kumuongeza mkataba na moja ya vitu vinavyojadiliwa na kuongezeka kwa mshahara wa mchezaji huyo .
0 comments:
Post a Comment