Katika mkataba wa ushirika huu , Real Madrid itafaidika kwa kupata mamilioni ya fedha ambazo zitatoka kwa benki hiyo katika utaratibu wa kawaida wa udhamini ambao klabu nyingi barani ulaya zinakuwa nao .
Ili kuwafurahisha washirika hawa wapya ambao ni watu wenye imani ya dini ya kiislamu klabu ya Real Madrid imeamua kufanya mabadiliko kwenye beji yake .
Mabadiliko haya yameshuhudia Uongozi wa Real ukiamuru kutolewa kwa msalaba ambao upo kwenye beji iliyopo kwneye jezi ya klabu hiyo lengo likiwa kuondoa mkanganyiko wa kiimani uinaoweza kujitokeza katika uhusiano kati ya klabu hii na wadhamini wake wapya .
Uhusiano huu ni muendelezo wa uhusiano ambao Real Madrid imekuwa nao na makampuni ya mashariki ya mbali ukiwemo mkataba wa udhamini wa jezi za timu hiyo ambao upo kati yake na kampuni ya usafirishaji wa anga ya Fly Emirates pamoja na kisiwa cha kifahari kilichopo huko Dubai ambacho kimejengwa kwa jina la klabu hiyo . .
0 comments:
Post a Comment