• OBAMA ataka chanjo ya EBOLA kushughulikiwa haraka

    Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI
    Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI amewataka wataalamu wa afya nchini humo wanaoshughulika na uvumbuzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA, kuongeza juhudi ili hatimaye chanjo hiyo iwafikie walengwa.

    OBAMA ametembelea taasisi ya ufumbuzi wa chanjo hiyo iliyoko huko MARYLAND, MAREKANI. Kiongozi huyo amefanya ziara hiyo, huku akitarajia kuwawishi wa bunge wa bunge la CONGRESS la nchi hiyo kupitisha muswada wa msaada wa dharura wa dola Bilioni sita za nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.

    Fedha hizo zitakwenda katika nchi za Afrika maghribi zilizoathiriwa na EBOLA kwa ajili ya ujenzi wa vituo zaidi vya afya. OBAMA amesema vita dhidi ya EBOLA haviwezi kuwa na mafanikio kama nchi zinazokabiliwa na ugonjwa huo hazitapata msaada wa kutosha hasa kutoka MAREKANI.

    Hata hivyo madaktari wasiokuwa na mipaka wamekuwa wakizilaumu serikali za nchi mbalimbali, ambako EBOLA bado ni tatizo kutochukua hatua madhubuti za kupambana na ugonjwa huo. Madaktari hao wanalalamika kuwa baadhi ya wauguzi wanaotumiwa kushughulikia wagonjwa wa EBOLA, hawana utaalamu wa kutosha wa kazi yao.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.