Henry ameichezea Red Bulls kwa muda wa miaka minne na nusu na inadhaniwa kuwa huenda akatangaza kustaafu soka baada ya kuwa kwenye mchezo huo kwa karibu miaka 20 .
Henry ambaye katika ubora wake aliwahi kuzichezea timu za As Monaco , Juventus , Arsenal na Fc Barcelona ukiachilia mbali timu ya taifa ya Ufaransa alinukuliwa akisema kuwa angependa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Arsenal ambako inaaminika kuwa atajiunga na benchi la ufundi chini ya kocha wake wa zamani Arsene Wenger .
Moja ya ishara zilizowapa watu sababu ya kuamini kuwa huenda kuna mpango wa nyota huyo kurejea Arsenal ni kitendo chake cha kubadili picha ya ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo alitoa picha inayomuonyesha akwia amevalia jezi ya New York Red Bulls na kuweka picha ya uwanja wa nyumbani wa Arsenal The Emirates Stadium .
Henry hadi leo anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya England katika historia ya ligi hiyo na amewahi kutwaa mataji karibu yote kluanzia kombe
0 comments:
Post a Comment