Gerard kimsingi anamaliza mkataba wake na klabu hiyo na ndani ya siku 31 zijazo atakuwa huru kuanza mazungumzo na klabu nyingine pasipo hata kuomba ruhusa toka kwa Liverpool kama ilivyo utaratibu wa mikataba .
Liverpool imepeleka ofa ya kwanza ya kumuongezea Gerard mkataba huku ikikanusha kuwa haijawahi kuzungumzia suala la kumpa mkataba ambao una thamani ya nusu ya maslahi anayoyapata kwa sasa .
Taarifa za Gerard kuongezewa kupewa ofa ya mkataba mpya ilifichuliwa na kocha wa klabu hiyo Brendan Rogers ambaye amesema kuwa Liverpool inafahamu mchango wa mchezaji huyo kwenye historia yake na haiwezi kumkosea heshima kwa kumpa ofa ambayo iko chini ya kile anachopata kwa sasa .
Kocha huyo wa Liverpool pia alikanusha habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati yake na Gerard baada ya kuvuma kwa habari kuwa nahodha huyo alikerwa na kitendo cha kuwekwa benchi kwneye mchezo dhidi ya Real Madrid huko Santiago Bernabeu na kwenye mchezo wa jumamosi iliyopita ambao Liverpool ilishinda 1-0 dhidi ya Stoke City .
Rogers amefafanua kuwa anafahamu kwamba Gerard ni mchezaji muhimu lakini hawezi kucheza mechi zote au dakika zote 90 kwenye kila mechi hivyo ni muhimu kupumzika kutokana na umri wake kuwa mkubwa .
Hata hivyo bado Gerard mwenyewe hajathibitisha kuwa atasaini mkataba mpya au la japo ishara zote zinaelekea nahodha huyo kusaini mkataba huo kutokana na mapenzi makubwa aliyo nayo kwa Liverpool ambayo ndio klabu pekee aliyoichezea tangu mwanzo wa maisha yake kama mchezaji na inatarajiwa kuwa atastaafu akiwa na klabu hiyo .
0 comments:
Post a Comment