![]() |
Lionel Messi |
Shirikisho
la Mpira wa miguu duniani Fifa limewataja Cristiano Ronaldo, Lionel
Messi na Manuel Neuer kuwania Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.Nyota hawa
watatu wameteuliwa toka katika kundi la Wachezaji 23 waliokua wakiwania
tuzo hii ya mchezaji bora itakayotolewa tarehe 12, Januari.
![]() |
Manuel Neuer |
Cristiano Ronaldo 29, atakuwa akiwania tuzo hii kwa mara ya tatu mara baada ya kuitwaa mara mbili.
Lionel Messi 27 akitaka kuweka historia ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya tano.huku kipa Manuel Neuer akiwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza na iwapo atatwaa tuzo hii ataweka historia kuwa mchezaji bora golikipa toka ilipowekwa historia na kipa Lev Ivanovich Yashin mwaka 1963.
Nyota wengine waliokuepo katika kinyanganyiro hiki kabla ya kuenguliwa ni pamoja na Angel di Maria,Eden Hazard,Yaya Toure,James Rodrigues,Zlatan Ibrahimovic ,Gareth Bale na Neymer.
0 comments:
Post a Comment