Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa majibu ya Serikali kuhusu ishu hiyo; “Mheshimiwa Mbatia jana ametoa malalamiko kuwa katika kadhia hii Polisi wametumia nguvu nyingi kuliko ilivyotakiwa, malalamiko haya ni mazito na Serikali haiwezi kuyafumbia macho, kwa hiyo pamoja na uchunguzi unaofanya na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ninaagiza idara ya malalamiko ndani ya Wizara kufanya uchunguzi kuhusu matumizi ya nguvu na ziada na ikithibitika kuwa kuna Polisi walitumia nguvu nyingi zaidi dhidi ya raia basi tutachukua hatua… Jeshi la Polisi halipaswi kutumia nguvu kuliko zinazohitajika katika kuwakamata watuhumiwa wa makosa ya jinai, halipo kwenye sheria, halipo kwenye Police General Orders“–
Waziri Mathias Chikawe.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe. |
“Serikali
inawaomba radhi wananchi wote waliokumbana na kadhia hii bila wao
kujihusisha na kuwasihi wananchi kujiweka mbali na matukio yote ya
uvunjifu wa sheria, Jeshi la Polisi halitamuogopa wala kumuonea haya mtu
yoyote yule litatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.
“Polisi
watumie nguvu stahiki kwa tukio stahiki.. Polisi wetu wanawajibu wa
kuwalinda Watanzania wote na mali zao zote, kwa nguvu zao zote“– Mathias Chikawe.
0 comments:
Post a Comment